Tuesday, December 9, 2014

PATA HABARI KUU KUBWA ZILIZOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO TZ

Nimekuwekea hapa mkusanyiko wa Stori zote kubwa muhimu kwenye Magazeti ya leo Tanzania Desemba 9, 2014


Nimekuwekea hapa mkusanyiko wa Stori zote kubwa muhimu kwenye Magazeti ya leo Tanzania Desemba 9, 2014

balNIPASHE
Zikiwa zimebaki siku tano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini,Katibu kata ya Kisutu,Dar es salaam kwa upande wa CCM Sauda Addy na mjumbe wa kamati ya udhamini ya Chadema Muslim Hassan wamepigana.
Sababu za kupigana kwao ni baada ya Hasan kudaiwa kuchana bango la mgombea huyo wa nafasi ya Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisutu ambalo lilibandikwa katika ofisi yake kwenye jengo la Shirika la nyumba NHC.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti na vyombo vya habari,Sauda aliyefika katika ofisi ya Hassan  kumshutumu kutokana na kitendo chake cha kuchana bango hilo.
Hassan alisema siku ya tukio Sauda alifika ofisini hapo na kuanza kumshambulia  kwa maneno na kipigo na watu kuamua kuingilia kati kuamulia vurugu hizo hali iliyosababisha kupoteza nyaraka zake za ofisini na kuharibu samani za ofisi.
Wote waliripotikatika kituo kidogo cha Polisi Kisutu na kutakiwa kwenda kuripoti katika kituo kikubwa cha kanda maalum ya Dar es aalaam ambapo walitakiwa kusubiri wakati upelelezi ukiendelea.
NIPASHE
Wimbi la Madaktari feki limezidi kushika kasi nchini baada ya daktari mwingine kukamatwa katika Taasis ya Mifupa na Mishipa ya fahamu na upasuajiwa Ubongo (MOI),Muhimbili jijini Dar es slaam.
Dakatari huyo alikamatwa jana ikiwa imepira miezi 10 tangu kukamatwa kwa mtu kama huyo katika hospitali hiyo ya Muhimbili.
Mtu huyo alikamatwa baada ya mwingine feki kukamatwa katika hospitali ya KCMC Moshi Septemba mwaka jana.
Aliyekamtwa jana alijulikana kama Dismas Macha mwenye miaka35 ambaye ni mkazi wa Upanga Magharibi jijini Dar es salaam ambaye ni mzaliwa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi mtendaji Athuman Kiloloma alisema daktari huyo alikamatwa na nyaraka mbalimbali za Moi na vifaa mbalimbali vya kutibia wagonjwa zikiwemo glovu.
MWANANCHI
Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe ameagiza kung’olewa kwa baadhi ya vigogo wa kampuni ya Reli Tanzania TRL ambao wanatuhumiwa kutumika kuhusika katika mchakato wa  wa ununuzi wa mabehewa ya kusafirisha kokoto kutoka India ambayo yalibainika kuwa mabovu.
Mabehewa hayo ni katiya 25 aina ya Ballist Hopper yaliyoagizwa nchini Julai 24 yakiwa yamegharimu kiasi cha bilioni4 na mengine 20 yalibainika kuwa ni mabovu na kulazimika kuanza kutengenezwa kwa kificho.
Mkataba wa kununua mabehewa hayo ulisainiwa mwaka jana Machi kati ya TRL na kampuni ya Hindusthan Engeneering ya nchini India.
Mwakyembe aligiza bodi ya Wakurugenzi ya TRL kuwasimamisha kazi mara moja kupisha uchunguzi,wahandisi wote waliokwenda India kwa ajili ya kufanya uhakiki wa ubora wa mabehewa hayo.
MWANANCHI
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewashangaa watu wanaotumia fedha na rasilimali za watu kwa ajili ya kuutaka urais  na kuwakumbusha wenye nia hiyo kuwa,Rais ni mipango na neema za Mungu.
Kauli ya Pinda imekuja ikiwani siku 1o tangu Spika wa Bunge Anne Makinda awaeleze Wabunge mjini Dodomana kujadili sakata la Escrow,kuwa waache kuingiza ushabiki wa kisiasa na kampeni za urais kwani ni Mungu pekee ndiye anayejua Rais ajaye.
Pinda alisema wanasiana wamekua wakifanya maamuzi bila kujali kuwa amani ndiyo ustawi wanchi na kuwalaumu wale wanaoutaka urais kwa gharama zozote.
Alisema uongozi wa nchi ni suala linalohitaji hekima  na ukemea tamaa.
MWANANCHI
Ikulu imesema pamoja na Rais kuwa tayari amepokea maazimio ya Bunge kuhusu wanaotuhumiwa uchotwaji wa mabilioni ya fedha za Escrow hawezi kuwachukulia hatua mpaka hapo uchunguzi kuhusu suala hilo utakapokamilika.
“Rais lazima aagize vyombo vya usalama kufanya uchunguzi kwa kina na baada ya hapo ndipo anapata mahali pa kuanzia,watu wengi wlaitaka Rais achukue maamuzi baada ya kupata ripoti hiyo jambo ambalo haliwezekani,”alisema Balozi Ombeni Sefue.
Alisema vyombo vinavyofanya uchunguzi kuhusu sakata hiloni vile ambavyo vilitajwa kufanya hivyo katika maazimio manane ya Bunge.
“Maazimio ya Bunge ni mazuri lakini inatakiwa muda kwanza ila rais naye apate  taarifa za uchunguzi zaidi,maazimio hayo ni muhimu na si ya kupuuzwa hata kidogo”alisema.
MTANZANIA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia wanawake wawili kwa tuhuma za kukutwa na mikia mitatu ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni74.2.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Leonar Paul pamoja na wanawake hao kukutwa na mikia hiyo walikamatwa pia na bundukimoja aina ya rifle na risasi moja.
Alisema  watuhumiwa hao walikamatwaDisemba 7 mwaka huu katika kijiji cha Ikuti Wilayani Ulanga.
“Watuhumiwa hao tunaendelea kuwahoji na watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa baada ya uchunguzi kukamilika”alisema Paul.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti, KUMEKUCHABLOG

No comments:

Post a Comment