Watu 37 wauawa Beni, ADF-Nalu yanyooshewa kidole

Usiku wa
Jumamosi Desemba 6 kuamkia Jumapili Desemba 7, watu wenye mapanga
wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF-Nalu, kwa mujibu wa viongozi tawala ,
walishambulia vijiji 3 wilayani Beni mashariki mwa jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na kuwaua watu 37 na kumjeruhi mtu mmoja.
Kwa
mujibu wa vyanzo vya RFI watu 37 waliuawa katika mashambulizi hayo,
ambayo yanadaiwa kutekelezwa na waasi wa Uganda wa ADF-Nalu wanaoendesha
harakati zao Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mashirika
ya kiraia mkoani Kivu Kaskazini yamesema kusononeshwa na mauaji hayo,
ambayo yametimiza idadi ya watu 250 kuuawa wilayani Beni kwa kipindi cha
miezi miwili. Watu zaidi ya 20,000 wameyahama makazi yao.
No comments:
Post a Comment