Staa huyu hakusubiri kupewa zawadi ya Xmas kutoka kwa mtu yoyote, kajinunulia mwenyewe zawadi hii…

Wengi tumezoea kupewa zawadi, lakini kumbe zawadi sio lazima kupewa hata wewe mwenyewe unaweza kujipa zawadi.
Msanii kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a Davido ameweka
picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha zawadi ambayo
amejinunulia kwa ajili ya Christmas ya mwaka huu na kuwashukuru
mashabiki wake waliomsapoti Duniani kote.
Amejinunulia gari aina ya Range Rover na
kuweka picha ya gari hiyo ikiwa na maneno haya; “EARLY CHRISTMAS
PRESENT FOR MYSELF!! BEEN A GREAT YEAR THANKS FOR ALL THE SUPPORT
WORLDWIDE! I WOULDNT HAVE GONE THIS FAR WITHOUT U GUYS!!


Hakika utapata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,Kumekucha blog
No comments:
Post a Comment