Picha za Harusi ya Kim Kardashian,Kanye West zaweka historia nyingine Instagram

Staa wa mitindo duniani pamoja na kuonekana kuwa kimya kwa sasa lakini ameonekana kuvunja rekodi katika mtandao wa kijamii wa Instagram kupitia picha zake za harusi na staa mwenzake Kanye West.
Wawili hao ambao ambao wamejali mtoto wa kike waliyempa jina la North,walifunga ndoa mwaka huu mwezi May na picha zao zilianza kusambaa mara tu baada ya kumalizika kwa sherehe ya harusi hiyo ya kifahari iliyofanyika nchini Italy na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali duniani.

Picha za mastaa hao zimeweza kutazamwa na watu wengi na zimetangazwa kama picha zilizopendwa zaidi ya mashabiki kwa kufikisha idadi ya watu milioni 2.4 mpaka sasa.
Kim Kardashian alionekana kuwa kimya baada ya hivi karibuni kupiga picha kwenye jarida la nchini Marekani zikimuonyesha akiwa mtupu na kuzungumziwa na mashabiki wake huku mumewe akionekana kutojali.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekuchablog
No comments:
Post a Comment