Unaifahamu timu yenye wachezaji wazee kuliko zote England?
Barani ulaya kila kitu hutawaliwa na tarakimu ambazo huwakilisha takwimu ambazo huhifadhiwa ili kuweka kumbukumbu ya jinsi ya kuendesha masuala mbalimbali kuanzia siasa , uchumi , biashara binafsi za watu na hata kwenye ulimwengu wa michezo .
Kwenye michezo takwimu ambazo zimezoeleka ni zile za kuonyesha jinsi wachezaji wanavyofanya kazi uwanja kwa maana ya asilia ya juhudi na mahali ambako kocha na wasaidizi wake wa masuala ya ufundi wanaweza kutambua ubora na udhaifu .
Hivi karibui takwimu zimeitaja klabu ya Manchester City kuwa timu ambayo ina wastani wa umri mkubwa kuliko klabu zote zinazoshiriki ligi za soka nchini England .
Takwimu hizi zimeonyesha kuwa Manchester City ina wastani wa umri wa miaka 28.8 kwa wachezaji wake umri ambao ni mkubwa kuliko klabu zote kubwa za ligi tano bora barani ulaya kwa maana ya Epl , Primera Liga , Serie A , Bundesliga na Ligue 1.
Kwa jumla Man City imeshika nafasi ya 7 katika utafiti uliofanyw akwa kutazama wastani wa umri wa wachezaji wa klabu zipatazo 500 barani ulaya kuanzia ligi kuu mpaka madaraja ya chini.
Manchester City ina wachezaji 12 ambao wana umri kuanzia miaka 29 kwenda mbele wakiwemo Kina Martin Demichelis , Frank Lampard ,Bacary Sagna , Yaya Toure , Gael Clichy , Jesus Navas na wengine .
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa Manchester City kwa timu za England ndio timu yenye wachezaji wenye umri mkubwa kuliko zote huku ikifuatiwa na Cyrstal Palace , Stoke City,West Bromwich Albion na QPR .
Kwa upande wa timu ambazo zina wastani wa umri mdogo ni Newcastle United , Manchester United , Southampton , Arsenal na Liverpool .
Ligi ya Italia Serie A inaonyesha kuwa ndio ligi yenye wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji wake huku ligi ya Uholanzi ikionekana kuwa ligi yenye wastani wa umri mdogo kwa wachezaji wa timu zake .
No comments:
Post a Comment