Friday, December 19, 2014

MAJAMBAZI WAVUNJA KIOO CHA GARI NA KUIBA MAMILIONI ZENJI

TUKIO LA UJAMBAZI,MLANDEGE ZANZIBAR JANA  KATIKA PICHA

MKUU wa Polisi Wilaya ya Mjini, Ali Makame (wa pili kushoto) akiangalia gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, muda mfupi baada ya kufika eneo la tukio katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar.ASKARI Polisi wakiwa wameizunguka gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar jana. Mmiliki wa gari hiyo aliegesha gari yake na kuingia msikitini kwa kusali sala ya Ijumaa katika msikiti jirani na maengesho ya gari katika eneo la mlandege.

No comments:

Post a Comment