Manchester City yafanya kufuzu ya karne.

Klabu ya Manchester City imezindua kituo chake cha kisasa ambacho kimegharimu paundi milioni 200 karibu na ulipo uwanja wake wa nyumbani wa Etihad.
Kituo hicho cha kisasa kina viwanja kadhaa vya nje na ndani huku kukiwa na sehemu kadhaa za kufanyia mazoezi kwa timu ya kwanza na timu za vijana .
Kituo hicho kina lengo la la kuhakikisha kuwa Manchester City inaondokana na utamadunia wa kununua wachezaji kwa bei ghali na badala yake kutengeneza nyota wake wenyewe ambao watakuwa wanaendelezwa kwenye kituo hicho .

Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Man City wakiwa kwenye eneo la kupumzikia wachezaji wakati wa mazoezi.

Ukuta unaoonyesha nukuu ya maneno aliyozungumza Sheikh Mansour wakati alipoinunua klabu hiyo mwaka 2008 .

Kocha
wa timu za vijana za Manchester City Patrick Vieira akiwa na mchezaji
wa zamani wa Arsenal Martin Keown wakiwa kwenye ziara ndani ya kituo
kipya cha Man City.


Beki
wa Manchester City Pablo Zabaleta akiwa kwenye uwanja wa timu ya vijana
ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 7000 kwa wakati mmoja .


Kituo hiki kinatimiza ahadi ambayo Sheikh Maosur aliiweka wakati alipoinunua Manchester City mwaka 2008 ambapo aliahidi kuwa atahakikisha anaijenga klabu hiyo na kuifanya kuwa klabu ya kisasa inayokwenda na wakati na si kuwa na kawaida ya kununua wachezaji nyota pekee.
No comments:
Post a Comment