Ulipitwa na 255 ya leo Desemba 8? Nimeirekodi na nimekuwekea hapa.

Kesi ya madai ambayo ilifunguliwa na
mganga Sheikh Shariff dhidi msanii AT inatarajiwa kutolewa hukumu ijumaa
hii ya tarehe 12 baada ya Mahakama kusikiliza pande zote mbili.
Kesi hiyo inahusu madai ya mganga huyo
kwamba alimtibia msanii huyo pamoja na kumpandisha nyota lakini msanii
huyo hakumlipa mpaka sasa.
Baada ya Mtanzania Idris kushinda
BBAHotshots 2014 siku ya jana imeonekana kama baadhi ya watu kutoka
Afrika Magharibi, akiwemo msanii wa Nigeria Davido kupost ujumbe Twitter
kuonesha kutoridhishwa na matokeo hayo japo muda mfupi baadaye aliufuta
ujumbe huo lakini bado watu ambao hawakupendezwa waliendelea
kumshambulia na wengine wakim-unfollow kwenye Twitter.
Diamond Platnumz ameshinda tuzo nyingine
Nigeria ambapo tuzo hiyo haikuwa ya kupigiwa kura, ambapo ilikuwa
inahusu msanii bora ambaye ameleta mabadiliko katika Sanaa Afrika.
Mastaa wengi walikuwa wakishiriki katika tuzo hizo ikiwa ni pamoja na mwanasoka Yaya Toure.
Sam Smith, Beyonce na Pharell Williams
wametajwa kuwannia vipengele sita katika Tuzo za Grammy ambazo
zitafanyika mwezi February mwaka 2015.
Uhusiano wa Chris Brown na Karrueche
huenda ukarudi kutokana na post ya Chris ambayo ameiweka mapema leo
kwenye ukurasa wa Instagram amemuomba radhi Karrueche na kuonyesha kuwa
yuko tayari kurudiana na mpenzi wake huyo
No comments:
Post a Comment