Kilio cha wakulima wa Karafuu Pemba
Kisiwa kidogo cha Pemba katika bahari ya Hindi, kilikuwa ndio walimaji wakubwa wa karafuu duniani kwa miaka mingi jambo ambalo lilikuwa likiwavutia watu mbalimbali wa mikoa ya jirani na nje ya nchi
Hivi
karibuni, nafasi hiyo h imechukuliwa na Indonesia. Wakulima
wa karafuu sasa wanasema wanahitaji serikali yao kuwasaidia zaidi ili
kuweza kuendeleza kilimo cha zao hilo walilolima kwa miaka mingi.
Wakazi wa Pemba na kisiwa cha Unguja pamoja na Serikali yao kipindi cha msimu wa Karafuu walikuwa wakikitangaza uvunaji wa Karafuu na kulazimika shule kufungwa ili kuwapa nafasi wananchi .
Hata hivyo baadhi ya duru mbalimbali wametoa malalamiko yao kwa Serikali kuliachia zao hilo lenye kuingiizia Serikali pato kubwa kuliachia na kutafsiri kuwa kuna walakini ndani yake juu ya wakazi wa Unguja na Pemba.
Kila mchumaji wa msimu wa Karafuu kisiwani humo aliweza kujipatia pesa nyingi hadi msimu kuisha jambo ambalo lilipunguza umasikini na kuwafanya wananchi kuwa matajiri na hata wale ambao waliweza kufika kisiwani humo maisha yao yamekuwa yakibadilika.
Karafuu inatumiwa duniani katika chakula, dawa na nchini Indonesia ni moja ya kiungo muhimu kwa utengenezaji wa Cigars.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment