Thursday, December 18, 2014

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO KTKA MAGAZETI YA LEO KWA HISANI YA MKOMBOZI SANITARIUM CLINIC TANGA

Mkusanyiko wa Stori zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 18, 2014 nimekuwekea hapa


Mkusanyiko wa Stori zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 18, 2014 nimekuwekea hapa

duniaa
NIPASHE
Jeshi la Polisi Wilayani Nzega,Mkoani Tabora limeaingia lawamani baada ya kumuua kwa kumpiga risasi tumboni iliyotokea mgongoni kijana mmoja aliyekua akisubiri matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Jumapili iliyopita.
Kijana huyo Batholomew Edward alipigwa risasi alipokua akisubiria matokeo hayo ya uchaguzi baada ya kundi la wanachama kuandamana wakipinga matokeo hayo.
Kamanda wa Polisi Tabora Suzan Kaganda alisema ofisi yake imethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kwamba ilikua ni bahati mbaya risasi ilimpata wakati askari wakipiga risasi za moto kujihami kutokana na waandamanaji kufanya vurugu.
Alisema siku ya uchaguzi wakati msimamizi wa uchaguzi akisubiriwa kutangaza matokeo mashabiki wa vyama walijikusanya na kuanza kurusha mawe baada ya kuona matokeo yamechelewa na kuharibu mali za Serikali.
Kutokana na hali hiyo Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi lakini wananchi hawakutii amri na ndipo walipoamua kutumia risasi za moto hewani na moja kumpata Marehemu Edward.
NIPASHE
Tanzania inakusudia kuzalisha umeme utakaotosheleza mahitaji ya Watanzania wote na ziada kwa ajili ya kuuza nje ya nchi ifikapo mwaka 2016.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la umeme nchini Felchesmi Mramba aliyasema hayo wakati wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo na kusema tayari Tanesco imeanza ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi ili uweze kutosheleza mahitaji ya nchi pamoja na ziada.
Alisema tayari awamu ya kwanza na ya pili ya mradi huo yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya Megawat 350 za umeme na imekamilika kwa asilimia 90 na inatarajiwa kuanza kazi ifikapo Machi mwakani.
Alisema awamu ya tatu na nne zitajengwa kwa ubia na kampuni ya Kichina ambayo itamiliki asilimia 60 ya hisa na Tanesco itamiliki asilimia 40 katika awamu ya tatu a ya nne itakua na mtambo wa kuzalisha Megawat 600 za umeme ambapo Tanesco itamiliki asilimia 30 na kampuni ya kichina asilimia 70.
MWANANCHI
Waziri mkuu Mizengo Pinda amekatisha kwa muda ziara yake katika Falme za kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais kwa shughuli maalum.
Waziri mkuu ambaye yupo katika ziara za kutembeleza nchi za Falme za kiarabu ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji,amekatisha ziara hiyo kwa siku mbili baada ya Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa za Escrow.
Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete kuridhia maamuzi yake huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya Mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa kwenye kashfa hiyo.
Kwa mujibu wa ziara hiyo Waziri mkuu leo alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembea maeneo mengine lakini ziara hiyo imevunjwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.
Baada ya kukamlisha jukumu aliloitwa,Waziri mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu jumamosi kuendelea na ziara yake.
MWANANCHI
Mamia ya wakazi wa jimbo la Arumeru Magharibi,jana walifurika katika mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa jimbo hilo,Joshua Nassar ya kuchoma bendera ya CCM yenye thamani ya shilingi 250,000.
Nassari alifikishwa katika mahakama hiyo saa 5 asubuhi akitokea rumande ya kituo cha Polisi Usa River ambako alilala baada ya kukamatwa juzi jioni.
Mbunge huyo alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,David Mwita kuwa alichana na kuichoma bendera hiyo juzi saa 11 jioni katika eneo la Maji ya Chai huku akijua ni kosa kisheria.
Hata hivyo Mbunge huyo alikana mashtaka hayo na aliachiwa kwa dhamana kutokana na mahakama hiyo kutokua na uwezo wa kutumia mawakili.
MWANANCHI
Kumeibuka Sintofahamu baina ya wafanyabiashara na wananchi wa maduka ya jumla na rejareja baada ya bei ya sukari kupanda gafla na kufikia 80,000 kwa mfuko wa kilo 50.
Hali hiyo imesababisha kilo moja iliyokua ikiuzwa kati ya 1600 hadi 1800 sasa kuuzwa 2000 katika maduka ya rejareja na taarifa za wauzaji zikisema bei itapanda zaidi wiki hii.
Sehemu kubwa ya Sukari inayouzwa Mikoa ya Kaskazini inatoka kiwanda cha TPC cha Mjini Moshia mbacho kimeweka wazi msimamo wake kuwa upungufu wa sukari umesababishwa na baadhi ya waagizaji wakubwa wa sukari ya nje ya nchi ili kuhalalisha hujuma.
Msemaji wa TPC Jaffar Ally alisema kuna vita kubwa kati ya wazalishaji wakubwa wa ndani na wafanyabiashara wanaoagiza sukari kutoka nje ya nchi.
HABARILEO
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mayala maarufu kama Flora Mbasha amefungua kesi ya madai  dhidi ya mume wake Emmanuel Mbasha kuomba talaka na kugawana mali walizochuma wakati wakiwa katika ndoa.
Flora alifungua kesi hiyo namba 64/2014 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam mbele ya hakimu Devotha Kisoka.
Pamoja na maombi hayo Flora aliomba aruhusiwe kuishi na mwanae Elizabeth Mbasha mwenye miaka 11 na kwamba Mbasha ahusike katika kumuhudumia mtoto huyo.
Flora alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu ameumizwa,amekua na msongo wa mawazo na kwamba anahitaji mtu atakayekua mwangalifu naye na kumsaidia.
Alieleza kwamba Mbasha alikua akimfanyia vitendo vya ukatili kwa kumshambulia kwa kipigo na baadaye kushindwa kutoa huduma na matibabu anapoumia na pia aliwahi kumtishia kumuua baada ya kuripoti ustawi wa jamii kuhusu mgogoro huo.
MTANZANIA
Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono wa CCM amenusurika kutekwa na watu wasiojulikana katika eneo la Tanki bovu jijini Dar es salaam.
“Nikiwa na msaidizi wangu tukitoka Bagamoyo tukiwa ndani ya gari langu aina ya Marcerdez Benz katika eneo la Tank bovu gafla yalitokea magari mawili na kutuziba kwa mbele lakini dereva baada ya kuona hali iyo aliondoa gari kwa kasi akipita pembeni na kufainikiwa kutoka eneo hilo”alisema Mkono.
Alisema baada ya kutoka eneo hilo magari hayo aligeuza na kumfuata yakiwa mwendo kasi na baada ya kuwafikia kijana mmoja aliyekua amevaa miwani nyeusi alishusha kioo na kututaka tusimamishe gari.
“Dereva wangu aliondoa tena gari kwa kasi hadi njia panda ya Kawe ambapo tulimkuta askari wa zamu na kumwelezea na kuomba msaada wake na baada ya muda kidogo magari hayo yaliwapita kwa kasi eneo hilo yakielekea Mbezi Beach na askari yule alitushauri kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi”alisema.
MTANZANIA
Walaji wa samaki wanaovuliwa kwa kutumia sumu wapo hatarini kukumbwa na matatizo ya ugumba kama uvuvi haramu hautatokomezwa haraka.
Imeelezwa kuwa samaki hao wakiwemo Sato na Sangara wanaovuliwa kwa sumu wana madhara makubwa kwa afya za binadamu  ikiwa ni pamoja na kukosesha nguvu za kiume na za kike pamoja na kuharibu mirija ya uzazi.
Mtafiti bingwa wa masuala ya mazingira kutoka kutoka Taasis ya utafiti nchini Godfrey Ngupula alisema athari nyingine zinazoweza kusababishwa na ulaji wa samakiwaliovuliwa kwa sumu ni pamoja na baadhi ya watoto kuzaliwa wakiwa wamedumaa kiakili na kuharibika kwa mishipa fahamu kwa kula samaki hao.
“Hatari mojawapo ni kupata ugumba,baadhi ya watoto kuzaliwa wakiwa wamedumaa akili na madhara mengineyo mengi.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment