Friday, December 19, 2014

TEKNOLOJIA YA KISASA KUEGESHA MAGARI YA BMW KWA KUVAA SAA YA SMARTPHONE

Habari njema kwa madereva…Sasa kuegesha magari yao kwa kutumia teknolojia ya saa


Habari njema kwa madereva…Sasa kuegesha magari yao kwa kutumia teknolojia ya saa

usukanHakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika eneo la kuegeshea magari.
Lakini sasa kero hiyo inaweza kubaki historia kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hiyo kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza kifaa hicho.
Hata hivyo dereva atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha anapotaka yeye.
bmw
Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.
Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hiyo ambayo itawezesha gari kujiegesha lenyewe na itaanza kufanya kazi mwezi ujao.
saa
Gari hilo linatumia miale aina ya Leser kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo na dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment