Nimekuwekea hapa mkusanyiko wa zile story kubwa kutoka kwenye Magazeti yote ya Leo Desemba 03 #Tz

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema wizi wa bilioni 306
kwenye akaunti ya Escrow ni matokeo ya nchi kuwa na Katiba isiyo na
vifungu vinavyozungumzia mambo hayo.
“.. Katika mchakato wa Katiba Mpya
tulisema kuwe na mgawanyiko wa madaraka na kila mtu ajue madaraka yake
ni nini na kutenganisha Serikali na Bunge…”
“… Kama Serikali na Bunge
vingetenganishwa na Bungeni usingeibuka mvutano kuhusu waliochota fedha
za Escrow. Bunge lingekuwa huru katika utendaji wake wa kazi…”
Alitaja Ibara ya 19 iliyokuwa katika Rasimu ya Katiba ambayo imeondolewa katika Katiba inayopendekezwa anayosema; ‘ Kiongozi
wa umma hataruhusiwa kutuhumiwa au hataruhusiwa kutumia au kuruhusu
kutumika kwa mali yoyote ya umma, zikiwamo zilizokodishwa kwa Serikali,
kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi au kumpatia mtu mwingine kwa
manufaa yoyote…”
MWANANCHI
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) mpya Profesa Mussa Assad ameapishwa jana Desemba 02 na
kuahidi kuanza kazi kwa moto sawasawa na ulioachwa na Mkaguzi
aliyestaafu, Ludovick Utoh.
Mkaguzi huyo ameahidi kuisimamia
Serikali na kulinda hadhi na heshima ya ofisi hiyo, aidha amesema
anasubiri kukabidhiwa rasmi taarifa ya Ripoti ya Escrow ambayo ina
taarifa ya maazimio ya Bunge ili aanze kuyafanyia utelezaji wa yale
yalioagizwa katika Ripoti hiyo.
Mstaafu wa nafasi hiyo, Ludovick Utoh
amesema amemkabidhi Prof. Assad ofisi ambayo ina watendaji wanaofanya
kazi kwa ari na ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na
kumkabidhi mwongozo maalum wenye kurasa 78 ambao una mwongozo wa
utendaji wa ofisi hiyo na yuko tayari kushirikiana naye wakati wowote.
Spika wa Bunge Anne Makinda amemwambia
CAG Assad kwamba kashfa ya Escrow imelifanya Bunge kujenga misingi
mizuri zaidi kiutendaji na uwajibikaji katika kuhakikisha matumizi
mazuri ya fedha za umma.
NIPASHE
Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
kimemtaka Naibu waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuwapatia shilingi bil.
16 kutoka kwenye pesa za Escrow ili watatue changamoto zinazoikabili
sekta hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Ezekiel
Ulouch amesema kiwango hicho cha pesa kitasaidia kutatua changamoto
kadhaa ikiwemo ya ukosefu wa madawati, kutekeleza muundo mpya wa walimu
na kuboresha mazingira ya shule.
TANZANIA DAIMA
Wanaume wawili katika Halmashauri ya
Busokelo Wilaya ya Rungwe wamefumaniana na kulazimika kubadilishana wake
zao baada ya kufanya makubaliano ya maandishi yaliyosimamiwa na
Serikali ya Kijiji.
Afisa Mtendaji wa Kijiji ambapo
limetokea tukio hilo amesema watu hao Paul Mboma alikutwa na Nuru
Sangwela, Ambakisye Mwakasege alikutwa na Lusie Lusepo ambapo kila mmoja
alikutwa na mke wa mwenzake na chini ya usimamizi wa Mtendaji huyo
wakakubaliana kubadilishana ambapo kila mmoja alimchukua mke wake na
wakasaini makubaliano hayo.
Wamesema kuwa maafikiano hayo yamefikiwa ili kuepusha urafiki wao usiharibike.
TANZANIA DAIMA
Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam
inawashikilia watu wawili Aboubakar Aman na Ezekiel Kasenegala kwa
mauaji ya wasichana wawili ambapo imesemekana wamekuwa wakiwalaghai
kimapenzi na kuwawekea dawa za kulevya kwenye vinywaji, na kasha
kuwabaka na kuwaua.
Wasichana waliouawa walikuwa wasichana
hao ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Ukutubi cha Bagamoyo, Wenze Makongoro
na Jackline Masanja na miili yao kutupwa katika maeneo tofauti Dar.
Kamishna wa Polisi Suleiman Kova amesema
watuhumiwa wamekutwa na nguo, hereni, mikoba na simu ambapo vyote
vilikuwa vinamilikiwa na marehemu hao.
Taarifa kuhusu vifo vya wasichana hao
iliwahi kuripotiwa na kituo cha Redio Clouds Fm wiki iliyopita katika
kipindi cha Hekaheka.
UHURU
Mafundi uashi wawili wamegundua mabomu
manane ya kutupwa kwa mkono ambayo inasemekana yamekuwepo ardhini kwa
Zaidi ya miaka 10 Kigoma kwenye Kijiji cha Mabamba walipokuwa wakichimba
msingi wa nyumba ya Mganga wa Kituo cha Afya.
Mafundi hao wamesema baada ya kubaini
kuwepo kwa chuma ambacho hawakukitambua waliamua kuoa taarifa Polisi na
Jeshi la Wananchi JWTZ, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari
Mohamed amethibitisha kutoa kwa tukio hilo.
Kamanda huyo amesema wanaendelea
kuwahoji wayu kadhaa ikiwemo Diwani wa wa Kata hiyo ambaye alikuwa
anaimiliki nyumba hiyo kabla ya kuiuzia Halmashauri ya Wilaya ya
Kibondo, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto amesema huenda mabomu
hayo yaliachwa na wapiganaji wa kutoka Burundi walipokuwa nchini kama
Wakimbizi.
Ni ahadi yangu kukufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, Kumekucha blog
No comments:
Post a Comment