Wasanii kumi wa Nigeria kwenye rekodi ya waliotafutwa zaidi kupitia Google Search
Mwaka unaisha, kwenye ule mfululizo wa rekodi mbalimbali za mwaka 2014 bado kuna nyingine nyingi millardayo.com itakuwa ikikupatia.
Tumezisikia rekodi nyingi za nje ya Afrika, sasa hivi moja ya jitihada ninazozifanya ni kukusanya zile rekodi za Afrika na kukuletea mtu wangu.
Davido ni mkoja ya mastaa ambao tukiuzungumzia muziki wa Afrika Magharibi, jina lake ni moja ya majina ambayo yameng’aa sana kwa mwaka 2014.
Mtandao wa Google umemtaja Davido kwamba ni staa namba moja kwa wanamuziki wa Nigeria aliyetafutwa zaidi mwaka 2014 kwenye mtandao.
Kwenye list hiyo Phyno ameshika namba mbili na nafasi ya tatu kushikwa na the Marvin’s Queen, Tiwa Savage
Nimekuwekea List ya top ten hiyo hapa.
1. Davido
2. Phyno
3. Tiwa Savage
4. Don Jazzy
5. Timaya
6. Ice Prince
7. Olamide
8. Sean Tizzle
9. Lil’ Kesh
10. Burna Boy
Unadhani ikija Tanzania nani ataongoza kwenye list hiyo? Nitafurahi ukiniandikia mtu wangu.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment