Hekaheka ya leo Desemba 09 inatoka Bukoba, inahusu Waumini kumkataa Mchungaji

Kama hukusikiliza Hekaheka ya leo Jumanne ya Desemba 9 kupitia Clouds FM kwenye Leo Tena, inahusu Waumini wa Kanisa la TAG
Bukoba kumkataa Mchungaji mpya aliyeletwa Kanisani hapo kwa madai ya
kumtaka Mchungaji aliyehamishwa na kupekwa sehemu nyingine arejeshwe.
Baada ya Waumini kumaliza Kuabudu kwa Nyimbo Mchungaji huyo Pius Alphonce aliinuka
na kuanza Kuhubiri ndipo baadhi ya Waumini walipoamka na kusema kuwa
hawawezi kuendelea na Mahubiri kutokana na watu wachache wanaotaka
kulivunja Kanisa hilo kwa maslahi yao binafsi, hivyo kutaka Mchungaji
wa zamani Erius Manoti aliyehamishiwa Karagwe arejeshwe.Hali hiyo ilipelekea mahubiri hayo kusimama na kuzuka fujo na kusababisha ibada hiyo kuahirishwa.
No comments:
Post a Comment