Thursday, April 30, 2015
MWALIMU ALIKACHA DARASA NA KUKIMBILIA KUUZA MITUMBA
Mwalimu kaona bora afanye biashara ya kuuza nguo kuliko hii ya kufundisha, kisa nini??
Kaskazini mwa Kenya hali sio shwari..
mara nyingi yameripotiwa matukio ya ugaidi, nakumbuka kuna tukio la basi
kutekwa watu wakauawa.. likatokea tukio jingine la wanafunzi zaidi ya
140 kuuawa katika shambulio la Chuo Kikuu Garissa.
Hii stori imeripotiwa leo na kituo cha TV cha K24..
mwalimu huyu alishuhudia lile tukio la basi kutekwa, wenzake waliuawa
huku akishuhudia.. hataki kurudi tena kufundisha, kaamua kuanza biashara
ya kuuza nguo za mitumba.
Japo analalamika kwamba kwa sasa hali
sio nzuri, kipato ni kidogo sana kwa sababu Serikali haimlipi tena
mshahara wake lakini hana jinsi, hawezi kurudi kufundisha sehemu ambayo
haina usalama.
FLOYD MAYWEATHER ADAIWA KUMKACHA MANNY PACQUIAO, APATWA NA KITISHO
Eti itawezekana Floyd Mayweather amkimbie Manny Pacquiao ??
Floyd Mayweather ana jukumu la kuuthibitishia ulimwengu kwamba yeye bado ni mbabe ambaye hataki kupoteza pambano lolote kwenye ulingo.. Manny Pacquiao nae ana jukumu la kukaza msuli ili ahakikishe anatengua rekodi ya Mayweather.. watu wanahesabu saa kadhaa tu historia iandikwe pale MGM Grand Garden Arena, Las Vegas Marekani.
Siku moja tu kabla ya pambano hilo kufanyika, kocha wa Pacquiao, Freddie Roach ametamka kuwa huenda Maywether akagoma kupanda ulingoni siku ya pambano hilo kwa kuwa anahisi Floyd hakutaka pambano hilo liwepo ila wamamlazimisha.
Mabondia hao usiku wa jana walikutana na waandishi wa habari na kuonyesha mkanda ambao mshindi atakabidhiwa baada ya mchezo huo.
Kwa pamoja
wamekutana na kila mtu ametoa ya moyoni, lakini kila mmoja kajigamba
kushinda pambano hilo.. tusubiri tu hiyo kesho usiku kutakuwa na majibu
gani ambayo dunia itayapata kutoka kwenye pambano.
TUTOKOMEZE VIFO VYA WAJAWAZITO
Wasanii wa kikundi cha Tanga kwanza
Entertaiment , Osward Raphael kushoto na Amina Juma , wakiigizo igizo wakati wa
uzinduzi wa mradi wa kupunguza vifo vya wanawake wajawazito vitokanavyo na uzazi Mradi unaotekelzwa na
Asasi ya Kiraia ya Tree Of Hope ya Tanga kwa Ufadhili wa Shurika Open Sociaty Iniative of East Africa
uzinduzi uliofanyika leo .
WASHABIKI AC WACHOSHWA NA BOSS WAO
Mashabiki wa AC Milan waja na staili mpya ya kukaa uwanjani… unajua kwa sababu gani?
Kutofanya vizuri kwa klabu ya AC Milan kumewafanya mashabiki wao kuingiwa na hofu na uongozi uliopo madarakani hadi kufikia hatua ya kuandamana.
Mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi ambaye
ameiongoza klabu hiyo kwa miaka zaidi ya 30 ameonekana kuchokwa na
mashabiki wa timu hiyo ambao sasa wameamua kufanya kama mgomo hivi ili
mmiliki abadilishwe kwa kuwa timu haijafanya vizuri kwenye matokeo ya
mechi zake nyingi.
Mashabiki hao wamekaa uwanjani kwa mtindo wa maandishi unaosomeka ‘BASTA‘ ambao tafsiri yake ni “sasa imetosha”.
Wengi wanataka kiongozi huyo aiuze klabu yake ili mtu mwingine atakayeinunua ifanye vizuri.
WATUHUMIWA KUIBA DUKA LA NGUO, KARIAKOO
Wanawake waliingia kwenye duka kama wateja, wizi uliotokea wanahusika nao??
Matukio ya wanawake kuiba kwenye maduka
ya nguo yanatokea sana Dar hasa maeneo ya Kariakoo.. kuna
dada mmoja aliwahi kukamatwa akapigwa na kuvuliwa nguo.. leo
inahusu wasichana watatu walioenda kuiba nguo kwenye duka moja maeneo ya
Magomeni Morocco.
Dada muuza duka amesema alikuwa
anawahudumia wateja wengine wakaingia wadada watatu waliovaa majuba na
nikabu.. baadae akaambiwa na mtu kwamba wanawake hao wameiba nguo wakati
yeye akihudumia wateja wengine.. watu wakawakamata lakini mmoja wao
alikimbia ambaye mashuhuda wanasema kuwa ndiye aliyeiba nguo hizo.
Wanawake hao walisema walikua wametoka
magomeni wakapitia dukani hapo lakini hawahusiki na wizi huo. Baadae
waliwapigia simu ndugu zao wakaja wakaomba ndugu zao waachiwe na wao
walikuwa tayari kulipa gharama ya nguo ambazo zimeibiwa na mmoja wa
wanawake hao ambae alikimbia.
Wanawake hao wamesema hawakuwa
wanafahamiana na huyo mwanamke aliyekimbia na nguo alizoiba hapo kwenye
duka.. wanasema wao walimkuta mwanamke huyo dukani kama ambavyo walikuta
wateja wengine.
VIMBWANGA VYA WALIMWENGU
Ndugu wamepeleka nguo za marehemu mochwari, ishu ni walichomkuta nacho baadae !!
Hii imeripotiwa toka Embu, Kenya..
nilipoiona nikadhani inafanana na ile ya Kibaha Tanzania ambako wezi
walivunja kaburi na kuiba mabegi ya nguo ambazo marehemu aliomba azikwe
nazo.. baada ya kuifatilia nikakuta hii iko tofauti kidogo, japo zote
zinahusu matukio wanayofanyiwa marehemu.
Familia waligundua kuwa mwili wa
marehemu ndugu yao umewekwa kwenye jeneza bila kuvalishwa nguo wala
viatu ambavyo walipeleka mochwari, lakini wafanyakazi wa mochwari
hawakumvalisha nguo hizo.
“Nguo
zenyewe tulikuwa tumeleta haziko kwa mwili.. mwili umewekwa mitumba,
tshirt ya mtumba, suruali ya mtumba hata viatu haikuwa imewekwa” alisema mmoja wa ndugu wa marehemu.
Baada ya ishu hiyo kuwa na mvutano
ilibidi ndugu wanunue nguo nyingine za kumvalisha ndugu yao, lakini bado
walibaki na maswali ambayo hayakuwa na majibu, nguo walizoleta mara ya
kwanza ziko wapi ??
AKUTWA AKIWA HAI BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI KWA SIKU 5
Kijana mwingine kakutwa hai baada ya tetemeko kuangusha Hoteli Nepal, unajua kafukiwa siku ngapi??
Pole kwa watu wetu Nepal, stori kutoka
huko ni za kusikitisha kwa zaidi ya wiki moja sasa hivi.. tangu
limetokea tetemeko watu zaidi ya 5,000 wamefariki, wengine zaidi ya
10,000 ni majeruhi.. hii ni idadi kubwa sana ya watu.
Kingine kilichopewa sana headlines ni kuhusu kuokolewa kwa kijana mmoja, umri wake ni miaka 15.. Pema Lama amekutwa akiwa hai, alikuwa amefukiwa na kifusi kilichotokana na kuanguka kwa jengo la ghorofa ambalo lilikuwa ni hoteli.
Kijana huyu kapatikana siku tano baada ya kutokea kwa tetemeko hilo.
Hii imerudisha matumaini kwamba katika
watu ambao hawajapatikana mpaka sasa huenda kuna watakaopatikana wakiwa
wazima.. kingine ambacho kilikuwa stori kubwa sana kwenye vyombo vya
habari duniani ilikuwa kupatikana kwa mtoto mchanga wa miezi minne..
mtoto huyo alifukuliwa toka kwenye kifusi akiwa hai siku ya Jumapili
April 28.
CHALSEA KUTANGAZA UBINGWA JUMAPILI STANFORD BRIDGE
Chelsea yaivua ubingwa Manchester City…
Ligi kuu ya England iliendelea tena usiku wa jana kwa mchezo mmoja kati ya vinara wa ligi hiyo Chelsea na Leicester City kuvaana.
Chelsea
ambao wapo kwenye mbio za ubingwa jana waliendeleza ubabe wao na
kujihakikishia nafasi nzuri zaidi ya kutwaa kombe hilo baada ya kuilaza
Leicester City mabao 3-1.
Ushindi huo umeiwezesha kufikisha pointi 80 wakati waliokuwa mabingwa watetezi, Man City wana pointi 67 na wakishinda mechi zao tatu zilizobaki watafikisha pointi 79.
Sasa Chelsea iliyobakiza mechi nne mkononi, inaendelea kushindana na Arsenal
ambayo iwapo itashinda mechi zilizobaki itafikisha pointi 82 hivyo
Chelsea inahitaji ushindi wa mechi moja tu kujihakikishia ubingwa.
Chelsea huwenda wakatangaza ubingwa Jumapili ya mwisho wa wiki hii kama watafanikiwa kuwafunga Crystal Palace katika dimba la Stanford Bridge.
SOMA MAKUBWA YALIOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO, APR 30 TZ
Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita wanaofanya mitihani ya Taifa. Kituo kimesajiliwa na NECTA. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
MTANZANIA
Sarafu mpya ya shilingi 500 inadaiwa
kuhujumiwa na baadhi ya watu ambao huinunua kwa Sh 2,500 na baadaye
kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha (silver).
Taarifa zinaeleza tangu sarafu hizo zilipotolewa kwa mara ya kwanza
Oktoba mwaka jana, baadhi ya watu wamekuwa wakizikusanya na kuzifanya
kuadimika mtaani.
Imeelezwa kuwa tangu kutolewa kwa sarafu hiyo imekuwa adimu mitaani
jambo ambalo si kawaida kwa fedha mpya zinazoingizwa kwenye mzunguko
kuadimika kwa kiwango hicho.
“Nimekutana na watu watatu wakitafuta
sarafu ya Sh 500 kwa Sh 2,500 hadi 5,000, mwanzoni nilipuuza lakini
baada ya kutulia na kufanya utafiti nimegundua kwamba kwanza hii sarafu
imekuwa adimu na inatafutwa kwa udi na uvumba,” kilisema chanzo cha habari jijini Dar es Salaam.
Meneja Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jovent Rushaka, alisema taarifa hizo wanazo na wanazifanyia kazi.
“Taarifa hizo tumezipata juzi na
tunalifanyia kazi suala hilo, kwa sasa tunafanya uchunguzi zinakofanyiwa
kazi, zinakouzwa ili tuweze kwenda katika maduka hayo na kufanya
uchunguzi,” Rushaka.
Katika hatua hiyo, meneja huyo aliwataka Watanzania kwa yeyote atakayebaini sehemu zinakotengenezwa na kuuzwa atoe taarifa.
Alipoulizwa kuhusu aina ya madini iliyotengenezewa sarafu hiyo ya Sh
500, alisema imetengenezwa kwa madini ya chuma kwa asilimia 94.
“Asilimia sita iliyobaki imetengenezwa
kwa madini aina ya nickel plated silver ambayo kidogo unaweza
kutengenezea mikufu ya ‘silver’. Sasa ni mtu gani anayenunua madini ya
chuma ni vigumu kuwezekana sasa, maswali ya kujiuliza ni je,
imetengenezwa na hiyo nickel plated silver?” alihoji Rushaka.
Alipoulizwa sababu za sarafu hiyo kuadimika imetokana na nini, alisema
BoT ilitoa sarafu hiyo tangu Oktoba mwaka jana na kwamba bado wanazo
nyingi.
Pia aliongeza kuwa Nickel sio miongoni mwa madini maarufu kwa ajili ya kutengeneza vidani vya thamani.
HABARILEO
Serikali imewasilisha mwelekeo wa bajeti
kwa Kamati ya Bunge, ambayo inalenga zaidi kupeleka umeme na huduma za
maji vijijini, kumalizia miradi ambayo haijakamilika na kutenga fedha
kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum
alisema wanaandaa bajeti ambayo itasaidia kumaliza mambo yote
waliyoahidi, ambayo yameainishwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo serikali iliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
“Bajeti
ya mwaka 2015/16 ni ya kipekee. Ni mwaka wa uchaguzi, ni mwaka ambao
serikali ya Awamu ya Nne inamaliza muda wake na serikali mpya kuingia
madarakani. “Ni mwaka ambao Mkukuta na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya
Milenia ya miaka mitano inafikia tamati, Malengo ya Milenia ya mwaka
2015 yanafikia ukomo na pia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama
Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 unakamilika,” alisema.
Akiwasilisha mwelekeo wa bajeti hiyo kwa
wabunge jijini Dar es Salaam jana, Mkuya alisema bajeti ya mwaka huu
imejikita zaidi kutathmini na kuangalia changamoto kwenye sekta ya maji, nishati, rasilimaliwatu na kumalizia miradi ambayo haijakamilika.
“Vipaumbele
kwenye bajeti hii vimejikita zaidi kwenye kuandaa awamu ya pili ya
Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano utakaoanza Juni mwaka 2016, na mkazo
zaidi ni kwenye miradi ya umeme vijijini, maji vijijini, kuimarisha
rasilimaliwatu na kugharamia uchaguzi mkuu,”Mkuya.
Akifafanua, alisema katika mwelekeo huo
wa Bajeti mpya ya mwaka 2015/16, jumla ya Sh takribani trilioni 23
zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika matumizi ya maendeleo na ya
kawaida.
Alisema katika matumizi ya
maendeleo,vipaumbele vitano ambavyo vimetajwa hapo juu (maji, umeme,
rasilimaliwatu, kumalizia miradi viporo na kugharamia uchaguzi mkuu).
Jumla ya fedha zilizotengwa ni Sh trilioni 5.8.
HABARILEO
Mwanafunzi wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert Mwakatenya anatuhumiwa kuuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert Mwakatenya baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa aliandikiwa na rafiki wake wa kike.
Mzazi huyo ambaye ni mfanyabiashara na
mkazi wa eneo la Majengo ‘D’ Manispaa ya Sumbawanga, anadaiwa kumwadhibu
mwanafunzi huyo, ambaye ni mtoto wake wa kwanza kwa kumpiga ngumi na
mateke mfululizo kwa zaidi ya saa tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda
alithibitisha tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili
iliyopita. Alisema bado wanamtafuta mtuhumiwa huyo kwani baada ya
kufanya kitendo hicho alitokomea.
Mwenyekiti wa Serikali Majengo D, Antony Nyambo alidai kuwa mzazi huyo alikuwa na tabia ya kumwadhibu mwanawe huyo, akimtuhumu kuwa ni mtoro wa shule .
“Nilitaarifiwa
juu ya kisa hiki Jumapili saa mbili asubuhi baada ya kutoka katika
ibada na raia mwema, ndipo niliamua kufika nyumbani kwa marehemu,
nilimkuta akiwa amelazwa chumbani, nilipomfunua niliona akiwa ametapakaa
vumbi mwili mzima huku akiwa amevaa nguo ya ndani tu,”
Inadaiwa kuwa usiku huo wa tukio,
mtuhumiwa alianza kumwadhibu kumpiga ngumi na mateke kuanzia saa mbili
usiku hadi usiku wa manane.
Mtoto huyo baada ya kupata kipigo hicho,
alizimia ambapo baba yake alimwagia maji mwilini hadi akazinduka, kisha
akamwamuru alale chumbani humo pamoja na mdogo wake.
Mzazi wa mtoto huyo alidamka alfajiri na kwenda kwenye chumba walicholala watoto hao na kugundua kuwa Jofrey alikuwa mfu.
“Ndipo
baba huyo alipoaga nyumbani hapo, akidai kuwa anaenda kutafuta gari ili
Jofrey aweze kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Mzazi huyo hakurudi
tena nyumbani kwake hadi sasa,” .
MWANANCHI
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema endapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
vitashindwa kuafikiana katika kuachiana baadhi ya majimbo kabla ya
Uchaguzi Mkuu, watawaeleza wananchi kwa kuwa ndiyo kiini cha kuanzishwa
kwa umoja huo.
Dk Slaa alisema hayo jana kabla ya
kumalizika kwa vikao vya wakuu wa Ukawa ambao wamekubaliana kusimamisha
mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani na kwa siku
mbili kuanzia juzi, walikuwa wakijadili ufanikishwaji wa azimio hilo.
Dk Slaa alisema hadi sasa
wameshakubaliana kuachiana asilimia 95 ya majimbo yote na kwamba ana
matumaini watafanikisha, lakini akaonya kuwa ikishindikana, hawatasita
kuwaeleza wananchi.
Mkoani Dar es Salaam, Ukawa imeshafikia
muafaka katika majimbo mawili ya Kawe na Ubungo na kubakiza majimbo
sita, wakati majimbo matano ya mikoa mingine bado yanaupasua kichwa
umoja huo wa vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD.
“ Ukawa ilikuwa ni ombi la Watanzania, ni sauti yao kwa hivyo taarifa zinazoendelea kutolewa siyo sahihi,”
alisema akirejea habari kuwa Ukawa, iliyoanzishwa wakati wa Bunge la
Katiba inaelekea kusambaratika kutokana na kushindwa kuafikiana kwenye
baadhi ya majimbo.
“Kama ikitokea tumeshindwa kufikia makubaliano mwisho wa safari yetu, hakuna kitakachokuwa siri, tutawaeleza Watanzania,” Dk Slaa.
Hata hivyo, alisema mpaka sasa hakuna
dalili zozote za umoja huo kushindwa kuafikiana kwa sababu ya mvutano wa
majimbo hayo, kwani mpaka sasa wameshafanikiwa kuyagawana kwa asilimia
95 nchini kote.
Habari za ndani kutoka katika vikao
hivyo zinaeleza kuwa uliibuka mvutano mkali kuhusu mgawanyo wa majimbo
17 yaliyobaki mpaka sasa.
MWANANCHI
Wakati Serikali imetangaza mapendekezo
ya mfumo wa mapato na matumizi yake kwa mwaka 2015/16 yenye vipaumbele
vinne, baadhi ya wabunge, akiwamo Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Dk Festus Limbu wameiponda wakisema haikuwashirikisha wadau katika uandaaji na kwamba haina kipya.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya alitaja moja
ya vipaumbele hivyo vinne kuwa ni Uchaguzi Mkuu, ambao awali alisema
haungekuwamo kwenye bajeti ya 2015/16 kwa kuwa fedha kwa ajili ya
shughuli hiyo zilishatengwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha
unaomalizika.
Vipaumbele vingine ni kuweka msukumo kwenye miradi ya umeme vijijini na maji vijijini na kuimarisha rasilimali watu.
Lakini Dk Limbu alisema Serikali
haikuwashirikisha wadau katika uandaaji wa bajeti hiyo ya Sh22.4
trilioni, wala kamati yake kabla ya kuja na mapendekezo hayo.
“Sisemi kwamba kazi yao ni mbaya.
Wamejifungia kule wakakamilisha kazi ndiyo wakaileta. Kwa mara ya kwanza
mimi kama mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti nimeikuta hii
‘figure’ ya Sh22.4 trilioni humu, nataka nieleze masikitiko yangu,”
alisema Dk Limbu.
Mwenyekiti huyo alisema Serikali ilipaswa kuwashirikisha ili kujaribu kupunguza mjadala mkali bungeni na kwenye kamati.
Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti hiyo
jana, Waziri Mkuya alisema Serikali imepanga kutumia Sh22.4 trilioni
katika bajeti ya mwaka 2015/16 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
miradi ya maendeleo ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 ya bajeti iliyopita
iliyokuwa Sh19.8 trilioni.
Kati ya fedha hizo, matumizi ya kawaida
ni Sh16.7 trilioni na matumizi ya maendeleo ni Sh5.7 trilioni, sawa na
asilimia 25.9 ya bajeti yote.
Alisema jumla ya mapato ya ndani
yanatarajiwa kuwa Sh 14.8 trilioni sawa na asilimia 57.8 ya bajeti yote.
Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya Sh13.3 trilioni
sawa na asilimia 90.1 ya mapato ya ndani.
Alisema mapato yasiyo ya kodi yatakuwa Sh949.2 bilioni na mapato kutoka vyanzo vya halmashauri yatakuwa Sh521.9 bilioni.
Aliongeza kuwa washirika wa maendeleo
wanatarajia kuchangia Sh1.8 trilioni katika bajeti sawa na asilimia 8.4
ya bajeti ikilinganishwa na asilimia 14.8 ya bajeti ya mwaka 2014/15.
Mkuya alisema Serikali ilipanga kutumia
Sh5 trilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika
bajeti iliyopita, lakini hadi kufikia Machi, mwaka huu ilikuwa imetoa
Sh2.4 trilioni tu.
NIPASHE
Machafuko ya kisiasa yanayoendelea Burundi, yamesababisha mamia ya raia wa nchi hiyo kukimbilia Tanzania kama wakimbizi.
Raia hao walianza kuingia nchini jana kwa ajili ya kutafuta hifadhi mkoani Kigoma
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilithibitisha kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 200.
Msemaji wa wizara hiyo, Isaack Nantanga, alisema kuwa wakimbizi hao waliingia mkoani Kigoma kupitia vijiji vya Kagunga, Kakonko, Kijaje na Chakeoya.
Nantanga alisema kuwa baada ya wakimbizi
yao kuingia katika maeneo hayo, maofisa wa Idara ya Uhamiaji walikuwa
wanaendelea na taratibu za kawaida za kuwapokea wakimbizi.
Mmoja wa maofisa Uhamiaji ambaye
hakutaka jina lake litajwe kwa maelezo kuwa siyo msemaji, alisema kuwa
wakimbizi 150 kutoka Burundi waliingia mkoani humo na walikuwa katika
kijiji cha Kagunga, wilaya ya Kigoma Vijijini.
Alisema kuwa maofisa wa Idara ya
Uhamiaji waliondoka jana kwenda Kagunga kuwachukua wakimbizi hao kwa
boti na kuwapeleka katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa ajili ya
kuwahifadhi.
Alisema kuwa watakaa kambini hapo hadi hali ya utulivu itakaporejea nchini Burundi.
Burundi imekumbwa na ghasia kutokana
na maandamano yanayofanyika katika mji mkuu, Bujumbura na wafuasi wa
vyama vya upinzani wanaopinga hatua ya Rais wa nchi hiyo, Pierre
Nkurunziza, kutaka kugombea tena urais, baada ya kumaliza muda wake wa
mihula miwili.
NIPASHE
Jumuiya na Taasisi za Kiisalam nchini,
imetoa tamko na kuipa serikali siku 15 kabla ya kufanya maandamano nchi
nzima kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakidai kufunguliwa kwa
madrasa zilizofungiwa kwa kuhusishwa na kutoa mafunzo ya ugaidi.
Masharti mengine ni kuachiliwa huru au
kwa dhamana masheikh na maimamu waliokamatwa wakituhumiwa kutoa mafunzo
na mazoezi ya kigaidi.
Maeneo ambayo madrasa hizo zaidi ya 10 zimefungwa ni katika mikoa ya Kilimajaro, Dodoma na Mtwara.
Tamko hilo pia lilisema jeshi hilo
linawatuhumu kwa kukusanya watoto na kuwafundisha elimu ya dini katika
mazingira yasiyofaa na kuwapo kwa taarifa za watu wenye milipuko
misikitini na kujihusisha na ugaidi.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikh Musa Kundecha, alisema jeshi hilo limekuwa likiwakamata watu hao usiku na kuwapeleka katika vituo vya polisi, na kuwahoji.
Alisema jeshi hilo limekuwa likifanya
kazi za maofisa wa ustawi wa jamii na elimu, kufanya ukaguzi katika
maeneo ambayo watoto hao wanafundishwa elimu ya dini ya kiislamu.
“Mkakati
wa operesheni hii unakiuka utu, haki za binadamu, kikatiba na ni
uchochezi dhidi ya Waislamu kuwafanya wachukiwe na jamii, tunawatunza
yatima katika maeneo jirani na madrasa na kuwapa elimu ya kidini siyo
kosa, tunatimiza wajibu wa kidini. Wajibu wa serikali ni kutulinda,
lakini tunawekwa katika mazingira ya hatari,” alisema Kundecha.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, alisema ulifanikiwa utafiti, kabla ya jeshi hilo kuchukua hatua za kufunga baadhi ya madrasa na kuwakamata watu hao.
“Katika
maeneo ya mikoa hiyo ni kweli kuna suala hilo, na watoto ambao wana
umri wa kuwa shule walikutwa pale, hivyo tukataka kufahamu na yajulikane
mafunzo wanayopewa,” alisema Nantanga.
Alisema kuendelea kushikiliwa kwa baadhi
ya watu waliokamatwa na kunyimwa dhamana kunatokana na jeshi hilo
kutojiridhisha au kutokamilika kwa taratibu za dhamana.
NIPASHE
Serikali imesema wafanyabiashara kugomea matumizi ya mashine za kielektoniki za ulipaji kodi (EFD’s), ni miongoni mwa sababu zilizokwamisha utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2014/15
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum,
aliyasema hayo jana wakati akiwasilisha mapendekezo ya mfumo wa mapato
na matumizi ya serikali kwa mwaka 2015/16, jana jijini Dar es Salaam.
Mwaka jana taifa lilikuwa na mgomo wa
wafanyabiashara nchi nzima, wakigomea mshine hizo kwa kile walichoeleza
bei zinazouzwa, mfumo uliotengenezwa unamfanya mfanyabiashara asione
faida bali mauzo ya siku.
Mara kwa mara walikuwa na mazungumzo na
serikali, lakini hawakufikia muafaka, na hadi sasa wachache ndiyo
wanaotumia mashine hizo.
Mwanzoni mwaka huu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Jonson Minja,
alikamatwa na polisi na kupelekwa mkoani Dodoma kwa kile kinachodaiwa
alikwenda kufanya mkutano wa kuhamasisha wafanyabiashara wa mkoa huo
wasitumie mashine hizo.
Baada ya kukamatwa wafanyabiashara waliendesha mgomo wa siku tatu wakilitaka jeshi la Polisi kueleza aliko kiongozi.
Waziri Mkuya alizitaja changamoto
nyingine za kibajeti kuwa ni serikali kulazimika kutoa fedha kwa
mashirika ya umma ya kibiashara kama Shirika la Ndege (ATCL), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), ambazo ziliongeza gharama ambazo zingepaswa kulipwa na mashirika yenyewe.
Nyingine ni mchakato mrefu wa kupata mikopo ya kibiashara.
Kuwa karibu nami kupata habari zinazojiri ndani na nje ya nchi ni hapa hapa tangakumekuchablog
FLOYD MAYWEITHER APATWA NA CHECHETO KWA PACQUIAO
HOFU YA FLOYD MAYWHEATHER KUJITOA KWENYE PAMBANO LA MANNY PACQUIAO YAZUKA
KOCH bora wa ngumi , Freddie Roach amnaye anamuandaa Manny Pacquiao kwa
pambano dhidi ya Floyd Mayweather Jumamosi wiki hii amezua hofu kuelekea mchezo huo wa karne.
Amedai kuwa yuko na wasiwasi Mayweather anaweza asitokee ulingoni kutokana na mgogoro wa glavu.
Mabondia
hao usiku wa jana wailikutana ukumbi wa MGM Grand ambao watapigana
Jumamosi katika Mkutano na Waandishi wa Habari kulitangaza pambano lao.
"Sifahamu kwa nini Floyd amekuwa mpole kwenye pambano hili. Nina wasiwasi kweli anaweza kujitoa usiku huo,"
amesema Roach.
"Anazungumza polepole sana. Kinyonge. Sifikiri bondia yeyote anaogopa, lakini sifikiri kama alilitaka hili pambano, alilazimishwa kwa pambano ambalo hakulitaka,"
amesema Roach.
Wednesday, April 29, 2015
AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG
Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita wanaofanya mitihani ya Taifa na wale wanaojiendeleza. Kituo kiko na walimu waliobobea katika fani ya Elimu. Kituo pia kinatoa huduma ya Hosteli. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
Subscribe to:
Posts (Atom)