Wednesday, April 22, 2015

AFRIKA KUSINI BADO HALI NI TETE

Bado mengine yanaendelea kusikika kuhusu Watanzania walioko South Africa..

South Africa immigrant attacksRaia wa kigeni waliokuwepo Afrika Kusini wengi wao wamejikuta wakilazimika kurudi kwenye nchi zao bila kupenda, hawakuwa na amani kutokana na machafuko ambayo yalitokea na kusababisha wengine saba kuuawa.
Kwa sasa hali ni mbaya na inadaiwa kuwa wageni wengi wameanza kuikimbia bila kupenda na kuacha mali zao zikiwemo majumba na rasilimali nyengine.
Hii imepelekea nchi kadhaa za Kiafrika kuwataka raia wao kurejea majumbani kwao.

No comments:

Post a Comment