Friday, April 24, 2015

HOTELI ANGANI (MAISHA)

Hoteli angani? ni Luxury private Jet ya kwanza ya Hoteli… nauli yake ndio noma.

picha 7Picha za kwanza za ndege binafsi inayotoa huduma za kihoteli zaidi angani zimetolewa na kampuni ya Canada ikiwa ni ndege inayomilikiwa na hoteli za Four Seasons.
Ni ndege iliyopangwa kifahari ndani yake na ina uwezo wa kubeba watu 52 kwa jinsi ilivyotengenezwa ndani yake na ikawa ina nafasi kwa kila mtu kukunjua kiti chake na kukifanya kama kitanda ambapo kama ingekua ni ndege ya kawaida nafasi hiyo ingefikisha viti karibu 150.
picha 6Wameanza kupokea oda za watu wanaotaka kusafiri na ndege hii kwenye nchi mbalimbali duniani ambapo safari ya kwanza itakua mwaka 2016 kuanzia Los Angeles na kuishia London ambapo gharama kwa kichwa ni USD 132000 zaidi ya milioni 250 za Tanzania ambazo zitajumuisha na malazi kwenye hoteli za Four Seasons kote itakapotua ambako ni Hawaii, Bora Bora, Sydney, Bali, northern Thailand, Mumbai and Istanbul.
picha 4
picha 3
Picha 2
Picha 1
picha 5

Kwa mambo mengi mazuri na yakusisimua usiwe mbali nami nitakupasha na kukuhabarisha mengi yanayojiri muda na wakati husika, ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment