Wednesday, April 22, 2015

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Leo mwanamke kasimulia kilichotokea hadi akaamua kuolewa mara ya pili

Lonely girl
Hii ni sehemu ya tatu ya ile Ishu ya mwanamke mmoja aliyeenda kuolewa kwa mara ya pili lakini ndoa hiyo ikazuiwa baada ya story kuvuja kwamba mwanamke huyo alikuwa anaolewa kwa mara ya pili.
Jana alisikika mume wa mwanamke huyo ambapo alisema hawakuwahi kuwa na ugomvi  katika ndoa yao ila alishangaa kuona mke wake anadai talaka ghafla bila sababu, baadae akasikia kwamba ameolewa na mwanaume mwingine.
Leo amesikika mwanamke huyo ambaye alitoka kwa mumewe na kwenda kuolewa mara ya pili, amesema walikuwa na mgogoro na mume wake wa kwanza wakaachana.. baadae akakutana na mwanaume wa pili, alihisi huyu ni kama anamdanganya.. wakaendelea na uhusiano baadae mwanaume huyo akamwambia kwamba anataka kumuoa, akaona akimwambia ukweli atamkataa.
Ishu ikamfikia mume wa kwanza, akaanza kumtafuta mwanaume huyu ambaye anamuoa mke wake na kumfanyia fujo.
Amesema ni kweli alikosea na yuko tayari kumuomba msamaha mwanaume anayemuoa mara ya pili lakini hayuko tayari kurudiana na mwanaume aliyemuoa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment