Friday, April 24, 2015

MUUMINI MWINJUMA ATOA YAMOYONI

Sababu ya  Muumini Mwinjuma akaamua kuanzisha Bendi yake..

549777-cool-drum-set-wallpaper
Msanii mkongwe wa muziki wa dance Mwinjuma Muumini ambae amesimulia yaliyomtokea mwaka 2002 akiwa kwenye bendi ya African Revolution.
Muumini amesema akiwa kwenye bendi hiyo kuna siku walikuwa wanafanya maandalizi ya uzinduzi wa album mpya wakati huo alikuwa anauguliwa na baba yake Bagamoyo na kumfanya ashindwe kwenda kambini kwenye mazoezi.. baadae akashangaa kusikia maneno kuwa anaringa, ilipofika siku ya uzinduzi akashangaa kupewa taarifa na Mwenyekiti wa bendi kuwa wanamuziki wenzake wamesema asije kwenye bendi, ishu hiyo haikuwa kweli.
IMG_0219
Siku ya uzinduzi akaamua kwenda ukumbini wakati bendi yake inafanya show.. mashabiki walipomuona hayuko kwenye stage wakaenda kumbeba na kumpeleka kwenye stage, ghafla uongozi uliamrisha mabaunsa wakamshushe, ikamtia aibu sana.. haikuchukua muda mrefu baada ya baba yake kufariki ndio wenzake wakaamini kuwa ni kweli baba yake alikuwa anaumwa, akaamua kujitoa kwenye bendi hiyo na kuanzisha bendi ya Double M Sound.

No comments:

Post a Comment