Idadi ya vifo vya watu iliyosababishwa na tetemeko la ardhi Nepal imeongezeka…
Jumamosi
iliyopita kuliripotiwa kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi katika
milima ya Everest huko Nepal ambapo si mbali na makazi ya watu.
Katika
tukio hilo watu mbalimbali walifariki, mpaka jana Jumapili April 26 watu
zaidi ya 2000 walikuwa tayari wamepoteza maisha huku majeruhi zaidi ya
5000 wakiripotiwa kuumia vibaya na kupelekwa katika hospitali
mbalimbali.
Habari
iliyoripotiwa hivi punde inaeleza kuwa idadi ya vifo hivyo imeongezeja
na kufikia 3, 351 na huenda idadi ikaongezeka wakati wowote kutokana na
majeruhi kuwa katika hali mbaya.
Mamia ya watu ambao wanaishi karibu na milima wanadaiwa kuwa katika hali mbaya na kukosa mahali pa kuishi.
No comments:
Post a Comment