Monday, April 27, 2015

UBISHI WA DEREVA WAGHARIMU MAISHA MAKUMI YA WATU, NIGERIA

Pole kwa watu wetu Nigeria.. Watu wamefariki kwenye hii ajali..

Kano-Collapse
Hii picha ya ajali nimeiona kwenye baadhi ya mitandao ya Nigeria, imenishtua nikaona niifatilie ajali imetokeaje.
Ajali imetokea Kano, Nigeria.. watu saba wamefariki, Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hili.. ajali hiyo imetokana na kuanguka kwa daraja la waenda kwa miguu lilil0kuwa likiendelea kujengwa katika barabara.
Mafundi waliokuwa wanajenga waliwakataza watu wasipite na magari chini ya daraja kwa sababu bado kazi ya ujenzi ilikuwa ikiendelea, huyo dereva wa taxi alikiuka agizo hilo.. alikuwa anakatisha na gari ikiwa na abiria, daraja likaanguka.. wamefariki watu saba..“– Magaji Majiya, msemaji wa Jeshi la Polisi.
d3
Daraja ambalo lilikuwa likijengwa lilikuwa kama hili.
Mara nyingi ujenzi ukiwa unaendelea kwenye barabara kunakuwa na vibao vya maelekezo lakini watu wengi huwa hawazingatii maelekezo, ndicho ambacho kimetokea kwenye hii ajali ya Nigeria.

No comments:

Post a Comment