Wednesday, April 22, 2015

AITWANGA RISASI 8 KOMPUTER BAADA YA KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Kompyuta yake iligoma kufanya kazi…maamuzi aliyochukua ni Stori

hasiraHii nayo inaweza kuingia kwenye headlines , sote tunafahamu kuwa kila mtu huwa na hasira pale anapokasirishwa na kitu fulani lakini  kitendo cha kuchukua maamuzi kwa lengo la kulipiza kisasi huenda kukaleta madhara zaidi.
Hii imetokea katika mji wa Colorado, Marekani ambapo jamaa mmoja Lucas Hinch amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kuipiga kompyuta yake risasi nane baada ya kushindwa kufanya kazi kama alivyotegemea.
Lucas alifikia maamuzi hayo ambapo aliipeleka kompyuta hiyo nyuma ya nyumba yake na kuamua kuipiga risasi bila kujua anavunja sheria na baada ya muda mfupi alikamatwa na polisi.
Inasemekana katika kompyuta hiyo herufi za ctrl+alt+delete zilishindwa kufanya kazi na ndipo alishikwa na hasira na kuamua kulipiza kisasi kwa kuiharibu Kompyuta hiyo hadi kiwango ambacho haiwezi kutumika tena

No comments:

Post a Comment