Wednesday, April 29, 2015

AJALI NYENGINE YATOKEA MORO JIONI HII

Bado tatizo la ajali TZ limeendelea kukaa kwenye headlines, hii imetokea leo Morogoro..

AJAStori za ajali Tanzania zimekuwa kwenye headlines nyingi.. cha kushtua zaidi ni kwamba ajali hizi zimetokea mfululizo sana, watu wengi wamefariki, wengine wengi majeruhi.. mara nyingi mwendo kasi umehusshwa sana na hizi ajali.
Leo iko hii kutoka Morogoro, watu 15 kujeruhiwa na wengine zaidi ya 50 wamenusurika katika ajali ya basi la Takbir lililokuwa likitokea Geita kuligonga basi la kampuni ya Abood katika eneo la Lubungo Mikese.
Majeruhi wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali ni  dereva wa basi la Takbir kutokuwa makini na kuendesha gari kwa mwendokasi.. baada ya ajali hiyo dereva huyo alikimbia.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment