Monday, April 27, 2015

MGANGA TAPELI AMTAPELI MAMA MMOJA MILIONI 1 NA SHILINGI MIA

Mama kafiwa na mtoto wake, akakutanishwa na mganga ambaye aliahidi kumrudisha.. Kilichofatia je??

Girl-Sitting-In-Sunset-Hd-WallpaperIliwahi ishu  inayofanana na hii ya leo yani mganga amedai anaweza kurudisha watu waliofariki.. ya leo ni kwamba mama mmoja wa Mabwepande, alifiwa na mtoto wake katika mazingira ya kutatanisha.. akakutana na mama mmoja ambaye alimwambia kuwa binti yake atakuwa amefariki kifo cha kishirikina, akamkutanisha na mama ambae aliwahi kurudishiwa mtoto wake.
Mama huyo amesema walianza mawasiliano, mganga huyo akamwambia atoe sh 100.. baadae walienda kwa mganga huyo Dodoma na kuoneshwa binti ambae aliona kama ni binti yake, mganga akataka allipwe sh. milioni mbili na shilingi 100 ili aweze kumrudisha.
Baadae walifika wakaoneshwa binti ambae hakuwa mtoto wake, mganga akawaambia kuwa binti huyo ameshamuweka kwenye gari lakini hawawezi kumuona hadi wakifika Dar.
Walipofika Dar hawakumuona mtoto kwenye gari, wakampigia simu mganga akawaambia waendelee kusubiri, baadae wakagundua kuwa jamaa hakuwa mganga ila ni tapeli.

No comments:

Post a Comment