Monday, April 27, 2015

ATEKETEZA GIOROFA , KISA WIVU WA MAPENZI

Ishu ilikuwa ni ugomvi wa wapenzi, ukawashwa moto mkubwa na kuchoma mpaka ghorofa na maduka..

flamesNimefikiwa na hii story kutoka Kenya,  inahusu mgogoro wa mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke.. mwanamke huyo amefariki, chanzo ni kwamba wapenzi hao walikuwa na ugomvi, mwisho wa ugomvi kukawaka moto mkubwa ambao uliteketeza  jengo la gorofa lililopo Kericho pamoja na vitu vingine kuungua.
Jamaa mmoja alifika kwenye duka lililoko kwenye jengo hilo na kummwagia mpenzi wake petrol aliyokuwa amebeba, halafu akajimwagia na yeye mwenyewe, akawasha moto wote wakaanza kuungua.. mashuhuda wamesema kisa ni mgogoro wa kimapenzi waliokuwa nao.
Akaanza kuwasukuma wateja waliokuwa katika M-Pesa akawaambia wacha nihudumiwe ndio akawasha kiberiti“, shuhuda aliyekuwa eneo la tukio.
Msichana huyo alifariki eneo hilohilo la tukio, jamaa ambaye alimlipua nae akapata majeraha makubwa na kupelekwa Hospitali ya Kericho, watu wengine wanne walijeruhiwa huku maduka kadhaa ya dawa na vitabu yakiteketea kwa moto.
Hii ishu ilikuwa kubwa sana, unaweza kuona hapa hali ilivyokuwa baada ya moto huo kuwashwa..

No comments:

Post a Comment