Monday, April 27, 2015

AMTWANGA RISASI TANO NA KUMUUA SIKU NNE TU YA NDOA

Siku 4 baada ya harusi, Mume kaamua kufanya ukatili huu wa kutisha kwa mkewe…

Handcuffed PrisonerWivu wa mapenzi upo, lakini huyu jamaa aliamua kufanya ukatili kwa mpenzi wake, ilikuwa siku nne tu baada ya kufunga ndoa zao.
Hii stori imetoka Brazil baada ya mume kuamua kumuua mke wake kisa tu huangaliwa na wanaume ikiwa ni siku ya nne tu tangu afunge naye ndoa kanisani.
Wawili hao ambao walikuwa wakiishi katika mji wa Rio De Janeiro, kwa sasa mwanaume huyo ameshikiliwa na polisi na kufunguliwa kesi ya mauaji.
Mwanaume huyo Vieira Severiano alimuua mkewe Cixera Alves De Sena ambaye alikuwa ni mcheza shoo katika bustani ya sehemu waliyokuwa wakiishi ambapo camera ziliweza kunasa tukio zima.
Video hiyo ilimwonyesha mwanaume huyo akigombana na mkewe kwa muda kabla ya kumpiga risasi tano usoni iliyosababisha kupoteza maisha yake.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment