Thursday, April 30, 2015

CHALSEA KUTANGAZA UBINGWA JUMAPILI STANFORD BRIDGE

Chelsea yaivua ubingwa Manchester City…

mooLigi kuu ya England iliendelea tena usiku wa jana kwa mchezo mmoja kati ya vinara wa ligi hiyo Chelsea na Leicester City kuvaana.
Chelsea ambao wapo kwenye mbio za ubingwa jana waliendeleza ubabe wao na kujihakikishia nafasi nzuri zaidi ya kutwaa kombe hilo baada ya kuilaza Leicester City mabao 3-1.
chelsea
Ushindi huo umeiwezesha kufikisha pointi 80 wakati waliokuwa mabingwa watetezi, Man City wana pointi 67 na wakishinda mechi zao tatu zilizobaki watafikisha pointi 79.
chels
Sasa Chelsea iliyobakiza mechi nne mkononi, inaendelea kushindana na Arsenal ambayo iwapo itashinda mechi zilizobaki itafikisha pointi 82 hivyo Chelsea inahitaji ushindi wa mechi moja tu kujihakikishia ubingwa.
chee
Chelsea huwenda wakatangaza ubingwa Jumapili ya mwisho wa wiki hii kama watafanikiwa kuwafunga Crystal Palace katika dimba la Stanford Bridge.

No comments:

Post a Comment