Friday, April 24, 2015

WENGI WAMTABIARIA PACQUIAO KUSHINDA

RAMBO: MAYWEATHER ATASHINDA PAMBANO DHIDI YA PACQUIAO!

Mabondia wa ngumi za uzito wa juu zaidi duniani, Floyd Mywether na Manny Pacquiao wanaotarajia kupanda uliongoni kuoneshana ubabe tarehe 2, Aprili mwaka huu.MCHEZA sinema maarufu duniani wa Marekani, Sylvester Stallone ‘Rambo’ amesema bondia Floyd Mayweather atashinda katika pambano dhidi ya bondia Mfilipino, Manny Pacquiao litakalofanyika Mei 2 mwaka huu.
Mcheza sinema maarufu duniani Sylvester Stallone 'Rambo' na bondia Manny Pacquiao.Hata hivyo, mtangazaji wa mapambano ya ngumi, Larry Merchant, alitofautiana na Rambo aliposema kwamba yeye anaweka kete zake kwa Pacquiao kushinda pambano hilo. 

Pambano hilo ambalo ndiyo ‘gumzo la mjini’ limeonyesha pia kwamba bondia maarufu wa zamani, Muhammad Ali, amesema mshindi atakuwa Pacquiao. Hii ni kwa mujibu wa binti yake aliyewaambia waandishi wa habari. Binti huyo, Laila, naye ni bondia Mmarekani ambaye alistaafu bila kushindwa.

No comments:

Post a Comment