Monday, April 27, 2015

MATUKIO YA KURUSHIANA RISASI BADO YAENDELEA MAREKANI

Baada ya ishu ya Lil Wayne kushtakiwa na dereva wake, risasi zimehusika tena kwenye msafara wake !

Buu
Matukio ya watu kuuawa kwa kupigwa risasi bado ni ishu ambazo zinasikika sana toka Marekani.. nyingine kubwa zilizochukua Headlines sana ni ishu ya Askari kuua raia, ikaenda mbali zaidi ambapo ishu hiyo ilihusishwa na ubaguzi wa rangi.
Leo story inahusu msafara wa tour ya Lil Wayne kushambuliwa kwa risasi na watu ambao bado hawajafahamika mpaka sasa.. mabasi mawili ambayo yalikuwa kwenye msafara huo wa Wayne ndiyo yaliyoshambuliwa, hakuna mtu aliyeuawa wala kujeruhiwa.
Ishu nyengine imetokea jana April 26 baada ya Wayne kumaliza kufanya show kwenye night club moja Atlanta, ndani ya mabasi kulikuwa na jumla ya watu zaidi ya 10 wa timu ya Lil Wayne lakini hakuna ambaye aliathirika kutokana na tukio hilo.
Moja kubwa ambayo ilikuwemo kwenye HEADLINES wiki moja iliyopita ilikuwa inahusu ishu ya Lil Wayne kushitakiwa na dereva wake wa zamani,  Mark Jones ambaye alidai kutishiwa bunduki na Wayne.

No comments:

Post a Comment