Friday, April 24, 2015

MAMA AVAMIA OFISI YA MKUU WA SHULE, KISA MTOTO WAKE ARUHUSIWE KUTUMIA SIMU SHULE

Mama wa mtoto hakuja shule kwa heri kabisa, kisa mtoto wake kazuiwa simu..

NoPhoneZoneIshu ya wanafunzi kuzuiwa kutumia simu au kwenda na simu shuleni hata kwa hapa TZ iliwahi kuwa mjadala mkubwa sana.. walimu walikuwa wakizuia wanafunzi kutumia simu ili kuwafanya wawe makini zaidi na masomo.. wanafunzi nao walisema wanataka waruhusiwe simu kwa sababu mawasiliano kwao ni moja ya vitu muhimu sana.
Nimekumbuka hilo baada ya kukutana na hii story toka India, mzazi mmoja hakupendezwa na suala la mtoto wake kukatazwa kwenda na simu shuleni, akavamia ofisi ya walimu na kuanza kumshambulia Mkurugenzi wa shule hiyo.
Mama huyo Taranjit Kaur Hundal aliingia kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Shule hiyo, Jyoti Nagrani na kufunga mlango kwa ndani alafu akaanza kumshambulia.. Tukio lote limerekodiwa kwenye video.
Mama huyo ambae ni mke wa mwanasheria ana kesi ya kufanya shambulio.
Huopitwa na habari inayonifikia na niko tayari kukusogezea muda na wakti wowowte kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment