Wednesday, April 22, 2015

SIO MTU, NI ROBOTI

Japan kwenye headlines nyingine tena.. Huyu ROBOT hana tofauti na mtu kabisa.. 

470502638
Bado dunia nzima inazungumzia teknolojia ya JAPAN, ile treni ambayo imevunja rekodi jana APRIL 21 kwa kutembea kasi ya kilometa 603 kwa saa, leo iko nyingine.. unajua tumezoea kukutana na yale masanamu kwenye maduka ya nguo, unakuta limevalishwa kabisa nguo.. vipi siku unakutana na sanamu la aina hiyo hiyo alafu linakusalimia au linakuongelesha???
GetimageasJpeg
Bado JAPAN imeendelea kukaa kwenye headlines.. ni upande huo huo wa teknolojia, mpya niliyokutana nayo leo ni hii ya robot ambalo linafanana kabisa na binadamu, tumezoea yale mengine ya kwenye movie ambayo mengi tunayaona ni marobot ya chuma hivi, hili liko kama binadamu.. ukikuta limesimama hivi hata huwezi kutofautisha na mtu wa kawaida.
hkg101038092_994818baff2bdae5389081248a07848f-nbcnews-ux-1160-900-640x0
Wajapan wamelipa robot jina la Aiko Chihira, lina uwezo wa kuongea, kusalimia, kuimba.. Kampuni ya Toshiba wamelitengeneza hili mwaka 2014 lakini Jumatatu April 20 2015 kwa mara ya kwanza liliwekwa dukani Tokyo, ilikuwa burudani yani watu wanasalimiwa kama wamekutana na mtu !!
Kwa sasa robot hilo lina uwezo kuongea lugha chache ikiwemo Kijapan na Kichina.

No comments:

Post a Comment