Thursday, April 30, 2015

FLOYD MAYWEITHER APATWA NA CHECHETO KWA PACQUIAO

HOFU YA FLOYD MAYWHEATHER KUJITOA KWENYE PAMBANO LA MANNY PACQUIAO YAZUKA

KOCH bora wa ngumi , Freddie Roach amnaye anamuandaa Manny Pacquiao kwa
pambano dhidi ya Floyd Mayweather Jumamosi wiki hii amezua hofu kuelekea mchezo huo wa karne.
  Amedai kuwa yuko na wasiwasi Mayweather anaweza asitokee ulingoni kutokana na  mgogoro wa glavu.
Kambi hizo mbili zinavutana juu ya glavu gani mabondia hao watavaa.
Mabondia hao usiku wa jana wailikutana ukumbi wa MGM Grand ambao watapigana Jumamosi katika Mkutano na Waandishi wa Habari kulitangaza pambano lao.
"Sifahamu kwa nini Floyd amekuwa mpole kwenye pambano hili. Nina wasiwasi kweli anaweza kujitoa usiku huo,"
amesema Roach.
"Anazungumza polepole sana. Kinyonge. Sifikiri bondia yeyote anaogopa, lakini sifikiri kama alilitaka hili pambano, alilazimishwa kwa pambano ambalo hakulitaka," 
amesema Roach. 

No comments:

Post a Comment