Wednesday, April 29, 2015

BREKING NEWS

Hatua moja mbele Jeshi la Nigeria.. Waliotekwa na Boko Haram wameanza kuokolewa

nigerian-special-forces
Kampeni nyingi zimefanyika duniani kulaani tukio la wanafunzi wa kike zaidi ya 270 kutekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ni mwaka mmoja umepita, wasichana hao walitekwa toka Shuleni Jimbo la Chibok, Nigeria.
Rais aliyechaguliwa kuongoza Nigeria, Rais Buhari moja ya vitu alivyosema ni kwamba hawezi kuahidi kwamba atahakikisha wasichana hao wanapatikana ila atafanya jitihada zote mpaka wapatikane.
cde42378-2688-46e1-a4cc-8e558cbbe70f-1020x612
Good news ya leo ni kwamba Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa wasichana 293 kutoka katika kambi za Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wasichana waliookolewa sio sehemu ya kundi la wanafunzi waliotekwa Shuileni, hawa ni wengine ambao wlaikuwa wakitekwa na Kundi hilo kila walipokuwa wakivamia vijiji mbalimbali vya kaskazini mwa nchi hiyo.
The-250-girls-are-being-held-by-Islamic-group-Boko-Haram-after-they-were-abducted-from-Chibok-in-north-eastern-Nigeria
Msemaji wa Jeshi la Nigeria amesema wanawake hao na mabinti walikutwa katika kambi nne tofauti baada ya Wanajeshi kuzishambulia kambi hizo.

No comments:

Post a Comment