Wednesday, April 22, 2015

NI VILIO TU KILA KONA

Najua kama uliziona hizi za ajali ya Basi Shinyanga utataka kupata taarifa kamili za ilivyokuwa.

Ajali 1Ni ajali nyingine iliyotokea Shinyanga na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwenye rekodi ya mwaka 2015 ikiambatana na nyingine nyingi zilizoua Watanzania ikiwemo ile ya Basi lililowaka moto.
Ni saa tisa kasorobo Alasiri April 22 2015 ambapo Basi la abiria la Unique aina ya Scania lililokua linaendeshwa na Issa Patrick (38) liligongana na Trela ambayo dereva wake amekamatwa na Polisi .
Polisi Shinyanga imesema watu tisa ambao ni abiria wa basi walifariki hapohapo na mwingine mmoja akafariki baadae na majeruhi ni 51 ambao walipelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
ajali 2Chanzo cha ajali ni dereva wa lori aliekua anatokea Nzega kuelekea Shinyanga kuendesha gari katikati ya barabara na akalishtukia basi wakati wameshakaribiana ambapo dereva wa lori alichoweza ni kutoa kichwa cha lori tu barabarani lakini Trela lililobaki kwenye barabara ndio likagongana na basi.
Kamanda wa Polisi amesema ni uzembe wa Madereva wote wawili kwa sababu pia walikua kwenye mwendo kasi,

No comments:

Post a Comment