Thursday, April 23, 2015

ALIEOLEWA MARA MBILI, MAMA MKWE AFUNGUKA

Ile ishu ya bibi harusi kuolewa mara mbili, leo mama mkwe kasimulia ilivyokuwa.

BrokenMarriageHii ni sehemu ya mwisho wa ile Ishu ya mwanamke aliyeolewa mara mbili, lakini ndoa ya pili ikazuiwa baada ya kugundulika kuwa mwanamke huyo alikuwa anaolewa kwa mara ya pili.
Alisikika mume wa mwanamke huyo ambae alisema hawakuwahi kuwa na ugomvi  katika ndoa yao ila akashangaa kuona mke wake anadai talaka ghafla.. akasikika  kwamba ameolewa na mwanaume mwingine.
Jana akasikika bibi harusi mwenyewe, akasema walikuwa na mgogoro na mume wake wa kwanza ambae baadae wakaachana akaamua kuanza uhusiano wa pili ambao ndio walikuwa wanaelekea kwenye ndoa.
Leo amesikika Mama wa bwana harusi ambae ndio aligundua ishu hiyo.. amesema alisikia maneno akiwa ukumbini kuwa kwa nini watoto wa bibi harusi hawajaenda kupiga picha na mama yao?baadae akaamua kumuuliza bibi harusi akakiri kuolewa na ana watoto 4 ila ameachika na eda haijaisha.
Mama anaendelea kusimulia kuwa walimtafuta mume wa kwanza wa mwanamke huyo akasema ni kweli wameachana lakini mwanamke hajamaliza eda.. wakaamua kufanya kikao na familia ya bibi harusi.. Sheikh aliyefungisha ndoa akamuuliza bibi harusi akakiri kuolewa ila ameachwa mwaka jana baba yake alipoulizwa talaka akasema anayo ila hakuja nayo na kuahidi kuwaletea kesho yake.
Wakamuita mume wake wa awali ambae walikuwa wamemficha akakiri kumpa talaka February 11 2015 na amezaa nae watoto 4.. ndoa yao wamekaa kwa miaka 16, Sheikh akawaambia kuwa ndoa hiyo ni batili.

No comments:

Post a Comment