Wednesday, April 29, 2015

MAYWEATHER AKAGUA UKUMBI WA PAMBANO LAKE KIMKWARA

Ni zamu ya Mayweather!! Hivi ndivyo alivyokwenda kukagua ukumbi wa pambano…(Pichaz)

bus
Siku mbili tu zimesalia kabla ya pambano la kimataifa la ngumi kati ya mastaa wawili Manny Pacquiao na Floyd Mayweather ambao watapanda ulingoni nakutegua kitendawili cha nani mkali zaidi.
weeHuku watu mbalimbali wakiweka mitazamo yao juu ya nani atamshinda mwenzake pia wapo mastaa mbalimbali kama 50 cent,P Didy ambao wameweza kuweka dau la fedha kati ya mabondia hao katika Pambano hilo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi duniani.
may2
Wakati homa ya pambano hilo ikizidi kupanda huku mabondia wote kila mmoja akimtambia mwenzake, jana tuliona PManny Pacquiao alivyowasili katika mji wa Las Vegas na familia yake pamoja na wapambe wake kwa mkwara, na leo ni zamu ya Floyd Mayweather ambaye ametumia muda wake kwenda kukagua ukumbi wa MGM Grand ambao utatumika kwa pambano hilo
may4
Mayweather wakati anakwenda kutazama ukumbi huo ulifurika mashabiki mbalimbali pamoja na camera za waandishi wa habari hazikuwa mbali kuchukua tukio zima.
warembo
Pambano hilo linatajwa kuwa pambano la kifahari zaidi duniani na ambalo viingilio vyake ni vikubwa ukilinganisha na mapambano mengine yaliyowahi kufanyika duniani.
wel
weza
Hutpitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment