Tangakumekuchablog
Muheza, MKULIMA
kijiji cha Bwembwera kata ya Amani Wilayani Muheza Mkoani Tanga, Yohana Msumari
(72) ameuwawa kwa kunyongwa hadi kufa na mfanyakazi wake kwa kile kilichodaiwa
kupunjwa maslahi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo, kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zubary Mombeji, alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 11 jioni, baada mtu aliedaiwa kuwa mfanyakazi wake kwenye
shamba la mahindi, Omary Choroghondo (36) kumyonga hadi kufa .
Alisema uchunguzi wa awali wa
kipolisi umebaini kuwa kwa kipindi
kirefu wawili hao wamekuwa katika ugomvi jambo ambalo mfanyakazi huyo kuchukua
maamuzi ya kumyonga tajiri wake hadi kufa eneo la shambani.
“Polisi inaendelea kumtafuta
mtuhumiwa kwa udi na uvumba ili kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma ambazo
zinamkabili----kitendo hiki cha maamuzi maovu hakiwezi kuvumiliwa” alisema
Mombeji na kuongeza
“Tunaendelea kufanya uchunguzi na
kuwahoji majirani na ndugu wa mtuhumiwa---jambo hili hatutaki kujitokeza tena
na tunataka kulikomesha” alisema
Katika tukio jengine kamanda
Mombeji, alisema mkazi wa Makorora Tanga, Helbert Mbwana, alifariki baada ya
kugongwa na gari wakati akiendesha baskeli eneo la Duga njia ielekeayo Pangani.
Alisema tukio hilo lilitokea juzi
saa 2 usiku wakati marehemu huyo akiendesha baskeli ambayo ilikuwa haina taa ya
kuonea na wakati akikata kona ilitokea gari na kumgonga na kufariki wakati
akikimbizwa hospitali.
“Marehemu wakati anakimbizwa
hospitali alifariki baada ya kuvuja damu nyingi kichwani---tatizo baskeli yake
ilikuwa haina taa na dereva wa gari kushndwa kumuona.
Kamanda alitoa wito kwa watumiaji wa
vyombo vya moto na watumiaji wa baskeli kuzingatia sheria za barabarani ikiwa
na pamoja na kuwa na taa ya kuonea nyakati za usiku ili kuepusha ajali
zinazoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment