Tangakumekuchablog
Lushoto,JESHI la
polisi Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, linamshikilia mkazi wa kijiji cha Shume
Tarafa ya Mlalo, Mwajuma Awadhi (25) kwa tuhuma za kuwauwa watoto wake wawili kisha kuwafukia katika shamba la mahindi.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zubeir Mombeck, alisema
tukio hilo lilitokea juzi saa 3 usiku na
kuwataja watoto hao kuwa ni, Zaina Khafidhi (4) na Mwanahamish Khafidhi (2).
Alisema kugundulika watoto hao
kulikuja baada ya wakulima waliokuwa wakielekea kondeni kusikia harufu kali na
kuifuata na kugundua kuzikwa kitu na kutoa taarifa kituo cha polisi Lushoto .
Alisema polisi ilifanikiwa kuifukua
na kukuta miili ya watoto wawili ikiwa imezikwa na kwenda kijiji na kubainika
kuwa watoto wao ni wa Mwajuma na kumsaka
hadi kumtia mikononi.
“Kwa sasa tunaendelea na uchunguzi
na mara baada ya kukamilika na
ikibainika mtuhumiwa tutampeleka mahakamani-----ni tukio la ajabu na halijawahi
kutokea kijijini hapo alisema Mombeck
Kamanda alisema uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa mama watoto huyo aliwahi kuugua kichaa na kuwa katika uangalizi
wa wazazi wake na jambo kwa kipindi chote hakuna taarifa zozote za matukio
mabaya aliyofanya.
Katika tukio jengine kamanda huyo
alilitaja kuwa polisi Wilayani Korogwe inawshikilia watu wanne kwa tuhuma za
kusafirisha mihadarati aina ya mirungi
kilo 446 katka kizuizi cha magari kijiji cha Makuyuni Wilayani humo.
Alisema tukio hilo lilitokea juzi
saa 8 mchana wakati wa upekuzi wa magari na kufanikiwa kukuta magunia mawili yaliyofichwa
katika uvungu wa basi la Ratco lililokuwa likitokea Arusha kwenda Tanga.
Alisema wakati polisi wakilifanyia
ukaguzi walisikia harufu kali mihadarati na ndipo walipozidisha upekuzi na
kuikuta ikiwa imefichwa chini ya uvungu wa basi hilo.
“Kutokana na kukithiri upitishaji wa
mirungi njia ya Kilimanjaro ndio maana kila gari lipitalo tunalifanyia upekuzi
wa hali ya juu---hii ni kutokomeza upitishaji wa madawa ya kulevya” alisema
Mombeck
Alisema kuanzia sasa polisi
watatumia vifaa maalumu vya kubaini madawa yakulevya na kufanya kazi usiku na
mchana kwani mbinu za wahalifu wamekuwa wakizitumia kwa nia tofauti.
Mwisho
No comments:
Post a Comment