Tangakumekuchablog
Tanga, WAZIRI
wa Wanishati na Madini, George Simbachawene, amewataka waagizaji wa mafuta na
gesi Tanga, kuacha kupandisha bei ya nishati hiyo kwa kisingio cha gharama na
badala yake kuweka unafuu ili kila mmoja kubadilika na kutumia nishati hiyo.
Akizungumza mara baada ya kufanya
ziara yake ya kutembelea bohari ya kuhifadhia gesi na mafuta kampuni ya mafuta
ya GBP na Like Ges, Simbachaweze amesema kuna baadhi ya makampuni hupandisha
bei kwa kisingizio cha gharama za uagiziaji.
Amesema kwa sasa jamii kubwa ya
Watanzania wametambua nishati ya gesi ndio matumizi stahiki na hivyo kuacha
kutumia mwanya huo kwa kupandisha bei na wananchi kushindwa kutumia.
Kwa upande mwengine Waziri huyo
amewataka wananchi kubadilika kwa madai kuwa nishati ya Gesi ndio matumizi ya
kimasikini na kusema kuwa matumizi ya
mkaa ni ya kiutajiri.
Mwisho
No comments:
Post a Comment