Unamfahamu Bingwa wa kadi za njano EPL?

Katika mchezo wa soka kuna kadi za aina mbili ambazo mwamuzi huwa nazo na hulazimika kumuonyesha mchezaji pale anapofanya kosa la aina Fulani.
Kwanza kuna kadi ya njano na kuna kadi nyekundu . Kadi ya njano hutolewa kama onyo na kama mchezaji ataonyeshwa kadi ya njano kwa mara ya pili kwenye mchezo mmoja basi atalazimika kutolewa uwanjani kwani kadi mbili za njano husababisha kadi nyekundu .
Wakati mwingine mchezaji anaweza kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na kutoka uwanjani kuendana ukubwa wa kosa alilofanya .
Katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya England mwishoni mwa wiki iliyopita mchezaji wa nafasi ya kiungo Gareth Barry alionyeshwa kadi ya njano katika mchezo dhidi ya timu yake ya zamani Manchester City .

Gareth Barry wa Everton akionyeshwa kadi ya njano kwa mara yake ya 99 tangu alipoanza kucheza kwenye ligi kuu ya England .
Gareth Barry ana nafasi kubwa ya kuzidi kadi alizoonyeshwa Davies kwani ligi ya England bado ina mechi 21 kabla ya kumalizika kwake na kama Barry atapata kadi moja ya njano atafikisha kadi 100.
No comments:
Post a Comment