Kile ambacho kimeamriwa kuhusu ule ugomvi uliozuka Bungeni Kenya…
Tume
ya Maadili na Kupambana na Rushwa Kenya (EACC) imeanzisha uchunguzi
dhidi ya Wabunge walioanzisha vurugu siku ya juzi December 18 katika
kikao cha Bunge maalum na kupelekea wabunge kadhaa kujeruhiwa, muda
mfupi baadaye Kikao hicho kikaahirishwa.
Mkuu wa Tume hiyo Mumo Matemu, amesema
kwa mujibu wa sura ya sita ya katiba kuhusu uongozi na namna ya
kujiendesha Wabunge hao walikiuka Sheria hiyo, hivyo tume hiyo imeamua
kulitathimini suala hilo na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika
katika vurugu hizo.
Vurugu hizo zilitokea baada ya pande
mbili za Chama Tawala na vyama vya Upinzani kushindwa kuendeleza mjadala
uliokuwa ukijadiliwa wa mapendekezo ya Sheria ya Usalama wa Nchi hiyo,
kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye masuala ya
Usalama.
No comments:
Post a Comment