Kutoka kwenye Magazeti ya leo December 20, Nimekuchambulia story kubwa tano kubwa, zisome hapa
MWANANCHI
Mahakama Kuu Dar es Salaam imewahukumu
kunyongwa washtakiwa sita, Mashaka Pastory, John Mndasha, Martime
Mndasha, Haji Kiweru, Wycliff Imbora na Rashid Abdikadir baada ya
kukutwa na hatia ya kupora pesa milioni 150/- za Benki ya NMB na mauaji
ya Askari wa FFU na mfanyakazi mmoja wa Benki hiyo.
Jumla ya vielelezo 78 vya ushahidi
viliwasilishwa Mahakamani mbele ya Jaji Projest Rugazia kwenye kesi hiyo
na kubaini washtakiwa hao walikuwa na hatia.
Washtakiwa hao walitenda kosa hilo siku
ya tarehe 20, 2006 ambapo uporaji wa fedha hizo pamoja na tukio la
mauaji lilifanywa na washtakiwa hao wakati walipokuwa wakisafirisha
fedha hizo kutoka Dar kwenda Morogoro.
MWANANCHI
Hospitali ya CCBRT na Chama cha Wamiliki
wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA) wamezindua kampeni ya kitaifa dhidi
ya Fistula ya uzazi ambayo lengo lake ni kusambaza taarifa kuhusiana na
ugonjwa huo na upatikanaji wa tiba yake.
Tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya ugonjwa huo wanawake zaidi ya 1,308 wamepata tiba ya ugonjwa huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Magreth Mhando
amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha mgonjwa wa Fistula
inatibika.
NIPASHE
Watoto watatu Rafael Bruno, Meshack
Gasper na Juvens Bathoromeo wamefariki kutokana na kuungua kwa moto
ambao waliuwasha kwa lengo la kuwinda wanyama katika msitu Kilosa,
Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro
Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo anasema moto
uliwazunguka watoto hao na kushindwa kupata mahali pa kutokea, mpaka
wakakutwa na umauti eneo hilo.
MTANZANIA
Kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka aliyoitoa juzi kwa vyombo vya
habari kwamba yeye na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo
hawatojiuzulu kwa kuwa Rais Kikwete anawategemea imeonekana kuwatibua
wasomi, wanasiasa na watu wa kada mbalimbali.
Baadhi yao ikiwemo aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu CUF, Julius Mtatiro aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa
Facebook uliosomeka hivi; “Hata kama
ulifeli magazijuto huwezi kujua fomula hii, kwa wanaojua maana ya
‘pre-emption’ watakubaliana nami kwamba taarifa ya Ikulu juu ya
Mwanasheria Mkuu kuachia ngazi iliyokuwa imejaa bashasha na sifa kuu
kwake ilikuwa na maana ya kuanza safari ya kulinda wezi wa fedha za umma.”
Mhadhiri na Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana amesema; “Nafikiri
Profesa anatakiwa kusoma alama za nyakati, anatakiwa kuona kwamba jamii
tayari imekwishahukumu, lakini pia anatakiwa kufahamu kuwa wakati
mwingine kama mwanasiasa unapaswa kuwajibika kwa ajili ya kujenga
heshima yako”
Bunge lilitoa maazimio ya kutaka watu
wanaohusishwa na uchotaji wa pesa za umma zaidi ya bili. 300 kwenye
akaunti ya Escrow kuwajibishwa ambapo mpaka sasa aliyekuwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema amejiuzulu.
HABARI LEO
Mabasi 11 ya abiria Lindi yamekamatwa na
SUMATRA kwa kutuhumiwa kupandisha nauli kutoka 22,000/- mpaka 35,000/-
kwa abiria mmoja kutoka Lindi kwenda Dar es Salaam.
Msimamizi wa SUMATRA Lindi, David Nyanda
amesema mabasi hayo yalipigwa faini y ash. 250,000/- kila moja huku
akiyataja mabasi hayo kuwa ni Mwana wa Mwanza na Machinga Bus.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment