Ifahamu timu yenye mashabiki wenye kelele kuliko wote nchini England .
Utafiti uliofanyika kwenye timu za soka nchini England ukiwaangalia mashabiki wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo umeonyesha klabu ambazo zina mashabiki wanaozipenda klabu zao kuliko wote.
Utafiti huo umeitaja Man United kuwa klabu ambayo mashabiki wake wanashangilia kwa kelele nyingi kuliko mashabiki wote hususan kwenye mechi za ugenini .
Pamoja na kutokuwa na mengi ya kushangilia baada ya timu yao kutofanya vizuri tangu alipoondoka kocha Sir Alex Fergusson bado mashabiki wa United wametajwa kuwa na sauti kubwa kuliko wapinzani wao kwenye mechi za ugenini .
Utafiti huu umeonyesha kuwa mashabiki wa United wanawazidi mashabiki wa timu za Newcastle United na Liverpool ambao wanafuatia kwenye nafasi ya pili na ya tatu kwa kelele zao wakati wakiwa wamesafiri kuitazama timu yao ugenini .
Klabu ya Arsenal imeshuka hadi nafasi ya saba hali ambayo huenda ikawa inachangiwa kwa kiwango kikubwa na mashabiki wa timu hiyo kuonekana wamemchoka kocha wao Arsene Wenger ambaye hivi karibuni alionekana hakubaliki mbele ya mashabiki wa timu yake kiasi cha kutengeneza mabango ya kutaka aachie ngazi .
Mashabiki wa timu zinazopambana kuepuka kushuka daraja kama vile Burnley na Queens Park Rangers kwa pamoja na west Bromwich Albion zimeoneka kuwa na mashabiki wasio na kelele wanapokuwa kwenye mechi za ugenini hali ambayo huenda ikawa inachangiwa na jinsi ambavyo timu zao zimeshindwa kupata matokeo mazuri ziwapo ugenini .
No comments:
Post a Comment