255 ya leo December 19 iko hapa, nimekuwekea hapa na unaweza kuisoma
Kundi la Jambo Squad wameamua kufanya wimbo mwingine waliomshirikisa Nakaaya ambao
una ladha ya kiutamaduni baada ya zile za kwanza kufanya vizuri, safari
hii wameamua kuachia wimbo ambao umeimbwa kwa lugha ya Kimeru ambao maana yake kwa Kiswahili ni salamu, ambapo wimbo huo unaachiwa kwa pamoja upande wa audio na video yake.
Msanii Izzo Bizness kwa mara ya kwanza amefanya video ya nyimbo nyumbani kwao Mbeya, ambapo amesema kuwa hii sio video official ya nyimbo hiyo ya Christmas na pia hana mpango wa kufanya video ya nyimbo hiyo kwa sasa.
Izzo amesema kuwa gharama ya video ni shilingi elfu arobaini tu, ambayo ni gharama ya taxi, watu waliohusika kushoot video hiyo hawakuhitaji malipo yoyote.
Izzo amesema kuwa gharama ya video ni shilingi elfu arobaini tu, ambayo ni gharama ya taxi, watu waliohusika kushoot video hiyo hawakuhitaji malipo yoyote.
Jokate ambaye amekuwa na madili mengi ya kijasiriamali kupitia brand name ya Kidoti amesaini
mkataba wenye thamani ya Sh 8.5 billion na kampuni ya Rainbow Shell
Craft Company Limited ya China kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa
mbalimbali zitakazokuwa na lebo yake ya Kidoti.
Albam ya msanii J Cole imeongoza kwa
kufanya mauzo makubwa sokoni japo albam hiyo aliitoa bila kurelease hata
nyimbo moja wala kuifanyia promo yoyote, huku nafasiya pili ikishikwa
na mauzo ya albam ya Rick Ross.
Kuisha kwa uhusiano wa Safaree na Nick
Minaj kunaonekana kumuumiza kila mmoja kwaupande wake kutokana na
Safaree kutishia kujiua huku Nick pia alionekana kuumizwa ambapo
alishindwa kumalizia Interview na kutokwa machozi baada ya kuulizwa
anavyojisikia baada ya uhusiano huo kufikia mwishoni.
Rapper Mase ameamua kudelete akaunti yake ya Instagram baada ya kupoteza followers
wake zaidi ya milioni moja aliokuwa nao kwenye ukurasa wake, ambapo
wamiliki wa mtandao huo wanaendesha kampeni ya kufuta akaunti fake na
akaunti ambazo zilifunguliwa na watu lakini hazitumiki.
No comments:
Post a Comment