HATIMAYE MWILI WA ASIHA MADINDA WAFANYIWA UCHUNGUZI KUZIKWA LEO MCHANA
Marehemu Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’enzi za uhai wake.
Baada ya
danadana nyingi, hatimaye mwili wa mnenguaji Aisha Madinda unafanyiwa
upasuaji muda huu katika hospitali ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Asha
Baraka amesema baada ya zoezi hilo, watauosha mwili wa marehemu katika
msikiti ulioko hapo Muhimbili ikiwa ni pamoja na uvishaji wa sanda kabla
ya kuelekea nyumbani kwao Kigamboni.Mazishi
ya Aisha Madinda yatafanyika Kigamboni makaburi ya Kibada leo mchana
muda wowote baada ya sala ya Ijumaa kutegemea na namna zoezi la
Muhimbili litakavyokamilika mapema.
fuatilia nini kitaendela na kumekucha blog
No comments:
Post a Comment