HDITHI HII INALETWA KWENU KWA HISANI YA MKOMBOZI SANITARIUM CLINC,TANGA WALIOKO CHUDA , TANGA
KISIWA CHA HARISHI
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
“Unahakika kuwa nitakuwa
salama?”
“Harishi hatakuja leo.
Ameshakuja asubuhi ni mpaka kesho”
“Ngoja niwaage wenzangu”
Tukatoka ukumbini. Wenzangu
walikuwa wameketi wakizungumza. Nikawambia kwa namsindikiza Yasmin.
“Ninakwenda kupika, nitampa
chakula awaletee” Yasmin akawambia.
“Yaani utasubiri chakula huko
huko?” Mmoja akaniuliza lakini uso wake haukuonesha furaha.
“Ndio atakisubiri” Yasmin
akamjibu.
Masudi akawatazama wenzake
kabla ya kuniambia.
“Sawa. Sisi tutasubiri”
Jina lake lilikuwa Masudi.
Katika sisi watu wanne tuliobaki, yeye alikuwa ndiye mkubwa kwetu kiumri.
SASA ENDELEA
Wakati mimi na Yasmin
tunatoka kwenye ile nyumba tukirudi nyumbani kwa Yasmin, Yasmin aliniambia.
“Yule kaka uliyezungumza naye anaitwa nani?’
“Anaitwa Masudi”
“Naona kama hakufurahi
ulivyomwambia tunatoka mimi na wewe”
“Inawezekana, ni binaadamu.
Labda ameona tumewabagua”
“Mbona wengine hawakusema
kitu?”
“Kila mtu ana mawazo yake.
Yule amezoea kutuamrisha kwa sababu kwenye kundi letu yeye ndiye mkubwa kiumri
na amekuwa kama kiongozi wetu”
“Kwa hiyo alitaka
anisindikize yeye”
Yasmin aliposema hivyo
nilicheka, na yeye akacheka.
“Unafikiri nakutania?”
aliponiuliza hivyo alitaja jina langu.
“Hunitanii, unaniambia
ukweli. Najua Masudi hakufurahi” nikamwambia.
Pakapita kimya kifupi kabla
ya Yasmin kuniambia.
“Kisiwa chote hilki kilikuwa
kina watu”
“Wewe uliwakuta hao watu?”
nikamuuliza.
“Wakati Harishi ananileta
hapa alikuwa ameshamaliza watu wote. Wengine walihama wenyewe kukimbia kifo”
“Na kama
leo anakuja na kutukuta hivi itakuwaje?”
“Atakukamata wewe.
Atakufyonza damu na ndio ataniuliza wewe ni nani na ulifuata nini hapa”
“Ina maana wewe
hatakuadhibu?”
“Ananitisha tu pale
ninapomuudhi lakini kama atanikuta na mwanaume
nadhani ataniadhibu”
“Lakini hatakufyonza damu?”
“Hapo siwezi kujua”
“Inatisha. Ni kwa vile tu
umenihakikishia kwamba hatarudi tena leo”
Tulipofika katika jumba la
Yasmin. Tulikaa katika ule ukumbi tukaanza kuzungumza.
Yasmin akanieleza wazi kuwa
alikuwa amenipenda.
“Wewe ndio ungefaa uwe mume
wangu” akaniambia kiudhati.
“Tayari umeshakuwa mke wa
jini, huwezi tena kuwa mke wangu”
“Jini amenioa wapi? Si
ananibaka tu!”
“Lakini ndio mume wako na
amekuleta huku kusudi aweze kukudhibiti”
“Hakuna kisichokuwa na
mwisho. Mwisho wake utafika tu”
“Inshaallah!”
“Mimi na wewe tutakwenda
kuoana Comoro!”
Nikatikisa kichwa changu.
Niliona Yasmin alikuwa anaota ndoto ya mchana.
“Yasmin huoni kuwa tuko jela!
Unawazia kwenda kuoana Comoro, hapa tutatoka vipi?”
“Tutatoka tu iko siku. Kila
siku mimi naswali kuomba”
“Angekuwa ni mwanaadamu
aliyekuweka hapa tungepambana naye. Lakini jini aliyemaliza kisiwa kizima ni
hatari”
“Usikate tama, usinivunje
moyo. Wewe mwanaume!” Yasmin aliposema hivyo alinyanyuka.
“Ngoja nikapike sasa”
akaniambia na kuelekea jikoni.
Wakati anatembea nilimtazama
kwa nyuma. Nguo alizokuwa amevaa zilimpendeza. Kama
alivyotueleza mwenyewe nguo hizo alikuwa naletewa na Harishi ambaye huziiba
kwnye maduka ya miji mikuwa.
Yasmin alipofika kwenye
mlango wa kuingilia ndani aligeuka na kunitazama. Alipoona nilikuwa namuangalia
akatabasamu kabla ya kuingia ndani.
Nilikaa peke yangu nikiwaza
hili na lile. Nilijiambia Yasmin alikuwa msichana mzuri, kikwazo kilikuwa ni
lile jini. Kama nafanikiwa kumuoa binti wa
rais ni heshima kubwa.
Baada ya muda kidogo
niliondoka nikamfuata Yasmin jikoni.
“Umenifuata huku?” Yasmin
akaniambia.
“Nataka tusaidiane kupika”
nikamwambia kwa mzaha.
“Si ungekaa tu nikakupikia
mume wangu mtarajiwa”
Nilijua Yasmin alikuwa
anajifariji kuniita “mume wangu mtarajiwa” Na mimi sikutaka kumvunja moyo. Kwa
upande mwingine mimi pia nilihitaji faraja kutoka kwa Yasmin.
“Hapana nataka nikusaidie
mtarajiwa wangu”
“Haya nisaidie”
Nikamsaidia Yasmin kupika
huku mizaha na dhihaka zikipita. Kwa mara ya kwanza niligundua Yasmin alikuwa
mchangamfu na aliyependa mzaha. Alikuwa akicheka hadi sauti yake ilisikika nje.
Alikuwa amesahau kabisa mateso yaliyokuwa yanatukabili sisina yeye.
“Yasmin unacheka sana, sauti yako inasikika
nje” nikamwambia.
“Kwani nani atatusikia, si
tuko peke yetu?”
“Najua tukompeke yetu lakini
usicheke sana”
ITAENDELEA KESHO
|
Thursday, December 18, 2014
KISIWA CHA HARISHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment