Friday, December 19, 2014

SOMA HABARI KUU ZILIZOJIRI KATIKA KURASA ZA MAGAZETI LEO KWA HISANI YA MKOMBOZI SANITARIUM CLINIC,TANGA

Mkusanyiko wa Stori muhimu zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 19, 2014


Mkusanyiko wa Stori muhimu zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya leo Tanzania December 19, 2014


RAUND
MTANZANIA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amesema hatojiuzulu kwa sasabu kufanya hivyo nifasheni.
Pamoja na kauli hiyo pia ameweka bayana kuwa yeye na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo wantegemea na rais Kikwete katika kumsaidia kufanya kazi.
Kauli ya Tibaijuka imekuja siku chache baada ya kujiuzulu kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema kutokana na kashfa ya uchotwaji wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow zaidi ya bilioni 300.
Waziri huyo alieza kuwa endapo uchunguzi utafanywa na kubainikakuwa fedha zilizoingizwa kwenye akaunti yake na mmilikI wa VIP Engineering James Rugemarila basi yupo tayari kuzirudisha.
Alisema anavishangaa baadhi ya vyombo na mitandao ya kijamii kwa kumwita Mama Escrow huku akiweka wazi kuwa yeye ni mama migogoro ya ardhi na si mama wa migogoro ya Escrow.
MTANZANIA
Serikali imetangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule mbalimbali nchini ambapo kati ya 451,392 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Ofisa wa Waziri mkuu Tamisemi Kassim Majaliwa kati ya waliofaulu mtihani hao ni wanafunzi 438,960 ambao ni sawa na asilimua 97.23 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Akifafanua kwa ambao hawakupangiwa alisema  9824 wanatoa Mkoa wa Dodoma,1,404 Dar es salaam,752 Morogoro,281 Mtwara  na 161 Katavi.
Alisema kutokana na uhaba wa miundombinu katika Sekondari nchini imewalazimu kuwaacha wanafunzi hao hadi pale Halmashauri husika zitakapokamilisha  ujenzi wa madarasa yanayohitajika.
MTANZANIA
Naibu Waziri wa Habari,Utamadunina Michezo Juma Nkamia amenusurika kupigwa na wananchi  jimboni kwake baada ya kutoa kauli zenye kejeli.
Nkamia ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Kusini alikumbwa na hali hiyo wiki iliyopita alipokua katika kijiji cha Nchemba alipokwenda kuwanadi wagombea wa CCM katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika wiki iliyopita.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho alisema Nkamia aliponzwa na kauli za kejeli alizozitoa dhidi ya aliyekua Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Msongozli Yahaya kutoka CUF.
Mkamia alimtuhumu Mwenyekiti huyo kwamba amekua akimchafulia mbele ya wnaanchi wake  kwa lengo la kumkwamisha katika uchaguzi ujao”Pamoja na kutoa maneno mengi ya kejeli hali ya hewa ilianza kuchafuka pale ambapo Nkamia aliagiza wasaidizi wake wamkamate mwenyekiti huyo aliyekua amekaa pembeni na kumpeleka katika gari lake.
Baada ya hali hiyo wananachi walianza kuzunguka gari la Nkamia  huku wakiwa na mawe ili kuhakikisha Mwenyekiti wao hakamatwi huku Nkamia akilizimika kuingia ndani ya gari na kuondoka kwa hofu ya kupigwa.
HABARILEO
Mwalimu wa chuo cha madrasa kilichopo Chakechake Pemba Said Khamis ameanza kutumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 15 jina linahifadhiwa.
Mwendesha Mashtaka wa Mapinduzi ya Zanzibar Ali Bilal aliiambia Mahakama mbele ya hakimu kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo miezi mitatu iliyopita.
Alisema baada ya ucgunguzi wa DNA uliofanywa Tanzania bara ulionyesha kuwa  asilimua 96 mtuhumiwa ndiye aliyempa ujauzito mwanafunzi huyo.
Alisema mtuhumiwa atatumia chuo cha mafunzo jela  kwa miaka saba na atakapotoka atalazimika kulipa fidia ya milioni moja ikiwa ni fundisho kwa wengine kuacha ufanya vitendo kama hivyo kwa wanafunzi wa vyuo na madrasa.
MWANANCHI
Mtanzania aishiye mjini Melbourne,Australia,Charles Mihayo aliyekua akituhumiwa kwa mauaji ya mabinti zake wawili,amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mihayo ametiwa hatiani baada ya Mahakama kujiridhisha kwamba aliwaua mabinti zake Indiana mwenye miaka mitatu na Savannah mwenye miaka minne kwa kuwabana  kwa mito ya kulalia na kukosa hewa.
Waendesha mashtaka walisema kwamba Mihayo amekiri kutenda kosa hilo na alitenda kosa hilo baada ya kuingia kwenye mgogoro na mkewe kwa ajili ya kulipiza kisasi.
Mahakama ilisema Mihayo alituma ujumbe wa maneno kwa mkewe huyo wa zamani akimwambia anahitaji kuwaona wa mara ya mwisho kabla ya kufanya mauaji hayo na alipowapeleka kwa ajili ya kuwaona aliwavalisha nguo mpya alizowanunulia.
Baada ya hatua hiyo inaelezwa kuwa Mihayo aliwapiga picha muda mfupi kabla ya kuwakweka pamoja na kuwabana pumzi kwa kutumia ito ya kulalia.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment