Thursday, December 18, 2014

MAXIMO HATAMBUI KUTIMULI AENDELEA KUICOCHI YANGA

Hii mpya ya Maximo nayo imemsuprise kila anaefatilia kufukuzwa kwake.

Maximo 1Mwandishi wa habari za michezo Saleh Ally (salehjembe.blogspot.com) ameripoti kwamba kocha Marcio Maximo ambae amechukua nafasi kwenye vyombo vya habari baada ya taarifa kwamba katimuliwa kwenye club ya Yanga, amewashangaza wengi baada ya kuibuka na kuendelea kuifundisha Yanga mazoezini.
Kocha huyo amefanya hivyo December 17 & 18 ikiwa ni sehemu ya kuonyesha hatambui suala la kuondolewa kwake kazin ingawa tayari alishafanya mazungumzo na uongozi wa Yanga kuhusiana na hilo, taarifa zinaeleza bado hajakabidhiwa barua rasmi.
Kocha huyo mbrazil na msaidizi wakeLeonardo Neiva waliendelea na kazi yao kama kawaida kwenye wwanja wa shule ya sekondari ya Loyola huku tayari kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi akiwa ameshawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mbrazil huyo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment