Kumekucha blog
Tanga, WASANII nchini wametakiwa
kuielimisha jamii kuishi kwa kuvumiliana na kusameheana kwa baadhi ya mambo hasa
kipindi hiki cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuelekea uchaguzi mkuu
mwakani kupitia nyimbo zao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa albamu ya pili ya msanii wa nyimbo za Injili, Magreth Singano ,
Askofu Mkuu na Mwasisi wa Huduma ya Evangelism and Prayer Ministry of Tanzania
(EPMT) Endrew Mhina alisema wasanii wako na nafasi kubwa kuielimisha jamii kupendana na
kuishi maisha ya kiucha Mungu.
Alisema kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi
mkuu mwakani wasanii wanatakiwa kutunga nyimbo ambazo zitaweza kuiunganisha
jamii kushirikiana katika mambo
mbalimbali na kuondosha tofauti za kiimani.
“Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuuu
mwakani niwaombe wasanii kutunga nyimbo ambazo zitawaunganisha wananchi na
kuondosha tofauti za kivyama” alisema
“Wasanii wako na nafasi kubwa ya kuwaunganisha Watanzania na niwaombe kutunga
nyimbo ambazo zitakuwa na faida kwa jamii---kuna baadhi wanashindwa kujitambua
na kutunga ambazo hazina faida” alisema Mhina
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, msanii Magret Singano
alikabidhi madawati 40 kwa shule ya msingi ya Masiwani kupunguza kero ya
uhaba kwa wanafunzi darasani.
Alisema mauzo ya albamu yake nusu atayapeleka katika kununua
madawati na kuyapeleka katika shule ambazo wanafunzi wake wanasoma chini lengo
likiwa ni kuisaidia Serikali katika jitihada zake za kuhakikisha shule zote
wanafunzi wanakalia madawati.
“Kupitia kazi yangu ya kuimba nyimbo za Injili na kuguswa na
elimu faida ya kazi yangu nitaipeleka katika elimu hasa upungufu wa madawati
kwa baadhi ya shule” alisema Singano
Aliwataka wasanii wenzake na wadau wa elimu kuchangia
madawati shuleni ili kuwawezesha watoto kuondokana na kero ya kusomea chini
jambo ambalo linachangia kupata matokeo mabaya mwisho wa mwaka.
Picha ya kwanza hadi ya tatu
Askofu wa kanisa la Magomeni Tanga, Ayuob Kuminambili akiliombea box lenye CD
za mwimbaji wa nyimbo za Injili, Magrert Singano kabla ya uzinduzi uliofanyika
juzi.
Picha ya nne
Askofu Mkuu na mwasisi wa Huduma ya Evangelism and Prayer Ministry of Tanzania (EPMT) akizindua
CD za mwimbaji wa nyimbo za Injli iliyobeba jinala Furaha na Shangwe ambayo ni
ya pili kuzindua.
No comments:
Post a Comment