Kama ulikuwa hujui ni lini mara ya mwisho Man Utd ilikua juu ya City kwenye EPL

Kama kuna kitu
kinasubiriwa kwa hamu na wanaolipenda soka duniani ni mechi ya mahasimu
wa jadi wa jiji la Manchester matajiri wa Manchester City dhidi ya
Manchester United weekend hii.
Kwa miaka mingi rangi nyekundu imekuwa
ikitawala hili jiji lakini lakini katika kipindi cha miezi 16 iliyopita
hali imekuwa tofauti, rangi ya blue imekuwa ikitawala jiji.

Hata hivyo kwa
mara ya kwanza tangu November 23 2013, Manchester United wataikaribisha
City Old Trafford wakiwa wapo juu ya Manchester City kwenye msimamo wa
ligi kuu ya England wakiwa wamecheza idadi sawa ya mechi.
Mara ya mwisho
kwa Man United kuwa juu ya City kwenye msimamo wa ligi ilikuwa baada ya
mechi 11 katika msimu wa 2013/14 wakiwa chini ya Sir Alex Ferguson
ambapo United walikuwa mbele ya City kwa pointi 1 kwenye msimamo.

Jumapili hii
timu hizo zinakutana Old Trafford huku Manchester United wakiwa mbele
kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 62 na wapinzani wao City wakiwa na
pointi 61.
No comments:
Post a Comment